
Na Mwandishi Wetu Tarime
Binti aliyetajwa kwa jina la Nyaroswe Mwita Magaiwa, 19, mkazi wa kijiji cha Genkuru, wilaya ya Tarime, mkoani Mara, ameripotiwa kujiua kwa kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani, kutokana na kinachodaiwa kwamba ni baada ya kupata matokeo mabaya ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne 2025.
“Binti huyu alikuwa akisoma Sekondari ya Bwirege, amejiondoa uhai kwa kujinyonga baada ya kupata matokeo mabaya ya mtihani wa kidato cha nne, na baada ya kuona wenzake wamefanya vizuri,” Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Genkuru, Juma Kegoye, ameiambia Mara Online News kwa njia ya simu, Jumatatu, Februari 2, 2026, bila kufafanua zaidi.
Mara Online News inaendelea na juhudi za kuwapata Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Tarime-Rorya, wazazi/ ndugu na uongozi wa Shule ya Sekondari Bwirege kwa ajili ya kuzungumzia kwa kina tukio hilo la kusikitisha.
Baraza la Taifa la Mitihani Tanzania (NECTA) lilitangaza matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne kwa mwaka 2025, juzi Jumamosi 31, 2026.
Social Plugin