EUNICE : MUME WA SAMIA ANGEKUWA NA WIVU TANZANIA TUSINGEKUWA NA RAIS MWANAMKE

Na Marco Maduhu,SHINYANGA
Diwani wa Viti maalum kata ya Lyabukande Eunice Magese

Diwani wa Viti maalum Kata ya Lyabukande wilayani Shinyanga, Eunice Magese, amewataka wanaume kuachana na mila kandamizi na wivu dhidi ya wake zao, na badala yake wawaunge mkono katika kugombea nafasi za uongozi, ikiwa ni pamoja na uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu.

Akizungumza kwenye mdahalo wa Shirika la WEADO uliofanyika leo Agosti 2, 2024, ulilenga kubaini vikwazo vya kijamii vinavyowakwamisha wanawake katika uongozi pamoja na  kuweka azimio la pamoja, mdahalo huo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa chukua hatua sasa zuia ukatili unaofadhiliwa na WFT-Trust.

Eunice amesema kuwa mume wake amekuwa msaada mkubwa katika safari yake ya kisiasa na kuweka wazi kuwa bila ushirikiano wa mumewe, labda asingekuwa diwani kwa miaka kumi.
“Wanaume, waacheni akina mama wagombee nafasi za  uongozi acheni wivu na mifumo dume, kama mume wa Rais Samia Suluhu Hassan angekuwa na wivu, Tanzania isingekuwa na Rais mwanamke,” amesema Magese.

Diwani mwingine wa viti maalumu, Zawadi Mwasha, amesisitiza kuwa ili mwanamke afanikiwe katika nafasi ya uongozi, ni lazima mumewe amuunge mkono. aliwaomba wanaume kutozuia wake zao kugombea nafasi za uongozi.
Diwani wa vitimaalum Zawadi Mwasha.

Mwalimu Upendo Dickson kutoka Shule ya Msingi Lyabukande amebainisha kuwa tatizo la kutojiamini kwa wanawake linatokana na malezi ya familia, ambapo watoto wa kike wanapewa nafasi chache na kupewa maagizo badala ya kuwa na uwezo wa kutoa maamuzi.

Wanaume na wazee maarufu wamehimiza wanawake kwamba wanaposhika nafasi za uongozi, kujiepusha na tabia mbaya na kuepuka kujirahisisha wanaposhawishiwa kushiriki mapenzi.

 Mzee maarufu Peter Amos amewasihi wanawake waliofanikiwa kuwa viongozi, kutoa semina kwa wenzao ili kuwawezesha zaidi katika kugombea nafasi za uongozi.
Afisa Tathimini na Ufuatiliaji kutoka Shirika la WEADO, John Eddy, alisema kuwa mdahalo huu ulifanyika kuhamasisha wanawake kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na uchaguzi mkuu mwakani, pamoja na kushiriki kupiga kura.

Veronica Masawe katibu wa Shy EVAWAC na Mjumbe wa bodi shirika wa WEADO, aliwashauri wanaume kuchunguza kwa makini taarifa mbaya zinazotolewa dhidi ya wake zao waliotangaza kugombea nafasi za uongozi, kwani mara nyingine masuala haya yanachochewa kisiasa kwa madhumuni ya kuwadhoofisha kisiasa.
Mdahalo huo umejumuisha watendaji wa vijiji, wenyeviti wa vijiji, viongozi wa dini, wazee maarufu, jukwaa la wanawake, vijana, maafisa maendeleo, walimu, na afisa elimu Kata ya Lyabukande.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Rasheeda Masawe akizungumza kwenye mdahalo huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Shirika la WEADO Eliasenya Nnko.

Tathimini na Ufuatiliaji kutoka Shirika la WEADO, John Eddy akizungumza kwenye mdahalo huo.
Tathimini na Ufuatiliaji kutoka Shirika la WEADO, John Eddy akizungumza kwenye mdahalo huo.
Veronica Masawe katibu wa Shy EVAWAC na Mjumbe wa bodi shirika wa WEADO akizungumza kwenye mdahalo huo.

Washiriki wakiendelea kuchangia mada kwenye mdahalo huo.

Washiriki wakiendelea na mdahalo.
Mdahalo ukiendelea.
Mdahalo ukiendelea.
Mdahalo ukiendelea.
Mdahalo ukiendelea.
Mdahalo ukiendelea.
Mdahalo ukiendelea.
Mdahalo ukiendelea.
Mdahalo ukiendelea.
Mdahalo ukiendelea.
Picha ya pamoja ikipigwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post