WAKULIMA WATAKIWA KULIPAISHA ZAO LA KARANGA




Na Dotto Kwilasa,Malunde Blog 1,Dodoma

Tanzania ikiwa kwenye shamrashamra za maadhimisho ya Maonesho ya Wakulima ambayo kitaifa yanafanyika Jijini Dodoma,imeelezwa kuwa Tanzaniani ni nchi ya pili kwa uzalishaji zao la Karanga Afrika baada ya nchi ya Nigeria huku Mkoa wa Dodoma ukitajwa kuwa kinara kwa uzalishaji wa zao hilo ikifuatiwa na Mtwara, Shinyanga na Tabora . 

Kutokana na hali hiyo, Wakulima Nchini wametakiwa kutumia maonesho ya Nanenane kujifunza mbinu za uzalishaji wa zao kwa kuzingatia kanuni bora ikiwemo kutumia mbegu zenye ukizani ili kuendeleza zao hilo kwa manufaa ya kibiashara.

Hayo yameelezwa leo Agosti 2,2024 na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Alssem Dkt, Emmanuel Monyo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika banda lao lililopo kwenye viwanja vya Nanenane Dodoma na kusisitiza wakulima kupanda mapema mbegu za zao hilo kwa kuzingatia kupanda katika nafasi zilizopendekezwa bila kusahau kupalilia kwa wakati ili kupata mazao mengi na Bora kuendana ulimwengu wa kidigitali.

"Mkulima ili aone tija ya kilimo chake ni vyema kuhakikisha anakausha mavuno mara baada ya kuvuna na Kuhifadhi mahali pasipo na unyevu, " amesema.
Ametumia nafasi hiyo kueleza umuhimu wa karanga kwa kueleza kuwa zao hilo ni la Mafuta ambalo hutumika kama chakula cha binadamu huku mashudu na majani yake kutumika kulisha mifugo.

Kwa upande wake Emmaculet Chaula ambaye ni mdau wa kilimo cha Katanga ametaja aina za karanga ambazo mkulima anapaswa kuzitumia kutokana na ubora wake kuwa ni Naliendela ambayo hukomaa kwa siku 90 Hadi 100 na mkulima akilima kutegemea kupata mavuno ya wastani wa tani 1 kwa hekta.

Aina nyingine ni Ndachi ambayo kukomaa kwa siku 110 na mkulima akilima kupata mavuno wastani wa tani 1.1-2 kwa hekta huku akiitaja mbegu ya Nari nut kustawi katika Ukanda wa chini na Kati na kukomaa kwa wastani siku 106 hadi 110 na inatoa mavuno ya wastani wa tani 1.3 hadi 2 kwa hekta.

"Nyingine ni Tanzanut,hii inastawi katika ukanda wa miracle 0 hadi 1500 kutoka usawa wa habari na inakomaa kwa wastani wa siku
116 na inatoa mavuno ya wastani wa tani 1.5 kwa hekta, wakulima wanapaswa Kuzingatia mbegu hizi ili kulima kilimo chenye faida, " amesisitiza





Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post