MR. MANGURUWE AIFARIJI FAMILIA YA MTOTO ASIMWE

Mkurugenzi kutoka kijiji cha Nguruwe kilichopo Zamahero Dodoma  Simon Mnkondya maarufu Mr. Manguruwe Juni 23,2024 amefanya safari kutokea Dodoma kuelekea Muleba mkoani Kagera katika kijiji cha Bulamula Kata ya Kamachumu yalikotokea mauaji ya mtoto mwenye Ualbino Asimwe Novath (2) kwa ajili kuipa pole familia ya Mama wa Marehemu Asimwe. 
Asimwe Novath enzi za uhai wake

Hivi karibuni Mwili wa mtoto mwenye Ualbino  Asimwe Novath  ambaye  alichukuliwa na watu wasiofahamika  nyumbani kwao  katika kijiji cha Bulamula kata ya Kamachumu ulikutwa ukiwa umetupwa kwenye karavati na kuondolewa baadhi ya viungo vyake vya mwili katika kijiji cha Marere kata ya Ruhanga wilaya ya Muleba.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post