HALI ILIVYO SOKO LA KARIAKOO WAFANYABIASHARA WAGOMA

Hali ilivyo katika mitaa mbalimbali ya soko kuu la Kariakoo asubuhi ya leo Juni 24 2024, wafanyabiashara wamegoma kufungua maduka wakishinikiza serikali kutekeleza makubaliano yao waliyokubaliana mwaka jana katika kikao chao na waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Baadhi ya wafanyabiashara wamesema sababu kubwa iliyopelekea wao kufanya mgomo huu katika Soko la Kariakoo ni TRA kurudisha enforcement kubwa zaidi kuliko ya awali iliyozuiliwa na Waziri Mkuu katika mkutano wa mwisho baina ya serikali na wafanyabiashara uliofanyika May Mwaka 2023 katika viwanja vya mnazi mmoja.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post