MAKONDA AMPONGEZA MKURUGENZI VANILLA INTERNATIONAL SIMON MNKONDYA ..."WATU KAMA NYINYI TUNAWATAKA"

Mkuu wa Mkoa wa Arusha  Mhe. Paul Makonda amempongeza Mkurugenzi wa makampuni ya Vanilla International na kijiji cha Nguruwe Zamahero Dodoma  Simon Mkondya kwa kufanikiwa kutatua na kuwekana sawa na wateja wake wawili baada ya kufikisha malalamiko katika ofisi ya mkuu wa mkoa.

Katika mkutano wa hadhara Simon Mkondya aliitwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda  ili kumaliza changamoto ya malalamiko yaliyowasilishwa ofisini kwake na wateja wake.

"Pole sana kwanza kwa kupata usumbufu huo mkubwa kwa kweli sisi tunaomba radhi kwa kukusumbua, sasa tungependa tukuokolee muda wako, Watu kama nyinyi tunawataka kwa sababu mnafanya shughuli kubwa, mnawekeza katika bara la Afrika na Vanilla tungependa liwe zao kubwa sana....mpigieni makofi ndugu yangu",amesema Mhe. Makonda.

TAZAMA VIDEO HAPA CHINI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post