RC FATMA AHIMIZA VIONGOZI WA DINI KUIMARISHA AMANI KWENYE MAENENO YAO


Mkuu wa mkoa wa Kagera Mhe. Hajat Fatma Abubakari Mwassa amekutana na kufanya Mazungumzo na Viongozi wa Misikiti (Maimamu) Kutoka Madhehebu ya Dini ya Kiislamu, katika Kikao maalum kilichofanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Kagera Aprili 04, 2024.

Katika Kikao hicho Mkuu wa Mkoa Hajat Mwassa ameendelea kuwasisitiza Viongozi hao kuendelea kuitunza Amani, na kujiepusha na Vitendo vyote vyenye kuashiria uvunjifu wa Amani, wakiwemo wale wanaogombea Uongozi (Uimamu) na Misikiti, na kuwa kwa sasa Serikali ya mkoa itakuwa tayari kumchukulia hatua  yeyote atayejaribu kufanya Vitendo vya uvunjifu wa Amani kwa kutumia mwavuli wa dini bila kujali dhehebu lake Wala Taasisi yake.

Mhe. Mwassa ameongeza kuwa  yamekuwepo makundi Fulani ambayo huchochea wenzao kuanzisha vurugu zisizokuwa na tija na kwamba anazo taarifa za kutosha kuhusiana na makundi hayo, ambayo ameyatahadharisha kutothubutu kwani Serikali haitosita kuchukua hatua juu yao.

Katika Kikao hicho Mhe. Mwassa amepata nafasi ya Kutoa Sadaka ya Futari kwa kutoka Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa  Kagera kwa Viongozi hao kwani wana mchango mkubwa hasa katika kipindi cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post