MBUNGE RWEIKIZA ATOA SADAKA YA FUTARI KWENYE MISIKITI 113 JIMBONI KWAKE BUKOBA VIJIJINI


Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini Dkt Jason Rweikiza ametoa Sadaka ya FUTARI kwenye Misikiti 113 iliyopo jimboni kwake.

Katibu wa Mbunge,Mhe Jason Lwankomezi amesema kuwa Futari hiyo itawafikia waamini  wa Dini ya Kiislaam kupitia Misikiti iliyopo katika maeneo yao.

Mhe,Lwankomezi amesema kuwa Futari hiyo ni Mchele pamoja na Sukari na walengwa ni waamini wote ambao wapo kwenye mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ikiwa ni desturi yake  yenye lengo la kuwafariji, kuleta umoja, upendo na mshikamano katika jamii.

Katibu wa Bakwata Wilaya ya Bukoba Vijijini Ndg,Ahmed Baitu amemshukru kwa Futari hiyo na kumsihi kuendelea kuikumbuka jamii yake.

Aidha naye Imam wa Msikiti wa Katoma Ndg,Yakub Abdallah Bishazo amesema kuwa kwa alichokifanya Dkt Rweikiza ni ishara ya kujali hivyo wanamuombea kwa mwenyezi mungu ili mambo yake yaendelee kuwa mepesi huku Mwenyekiti wa Vijana Bakwata Bukoba Vijijini Ndg,Shafi Abudkadri Kwa niaba ya vijana amemshukru sana Mbunge huyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post