WANANCHI WAFUNGA BARABARA YA MWANZAA - SHINYANGA KUKITHIRI MATUKIO YA AJALI UGWETO , WATU WAWILI WAMEGONGWA LEO

Wakazi wa kata ya Bugweto manispaa ya Shinyanga wamelazimika kufunga barabara kuu ya Shinyanga - Mwanza baada ya leo watu wawili waliokuwa wamepanda kwenye baiskeli kugongwa na gari na kusababisha kifo cha Daudi Kulwa Mwandu (25) mkazi wa Bugweto na mwingine Athuman Mtatiro Wambura (33) mkazi wa Tambukareli kujeruhiwa.

Wakizungumza na Malunde 1 blog wananchi wamedai ajali nyingi zimekuwa zikitokea kwenye barabara hiyo zikisababishwa na mwendokasi unaosababishwa na baadhi ya madereva wa magari.

Baadhi ya wananchi wamedai kuwa ukosefu wa kizuia mwendo (matuta) kwenye barabara hiyo na baadhi ya madereva kutofuata sheria za usalama barabarani imekuwa chanzo cha kusababisha vifo vitokanavyo na ajali.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga ACP Janeth Magomi amefika eneo la tukio na kuzungumza na wananchi hao ambapo amesema wataendelea kuimarisha doria za usalama barabarani katika eneo huku katibu tawala wilaya ya Shinyanga Said Kitinga amefika na kuchukua hatua kwa kuzielekeza mamlaka husika.
Msafara wa magari yakiwa yamezuiwa.





Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post