AFISA MKUU WA FEDHA - ANGLOGOLD ASHANTI ATEMBELEA GGML


Gilbert Chamlonde, Meneja – uchimbaji wa kina kifupi juu ya ardhi akitoa muhtasari wa historia ya uzalishaji wa mgodi wa Nyamulilima kwa Afisa Mkuu wa Fedha wa AngloGold Ashanti, Gillian Doran.
Mhandisi wa GGML anayedhibiti ubora na viwango vya miradi, Maftah Seif akitoa maelezo zaidi kuhusu teknolojia ya hali ya juu itakayotekelezwa katika kituo kipya cha GGML chenye uhusiano na TANESCO. Mradi huu ni ushahidi wa juhudi za GGML zinazoendelea za kuboresha kuongeza ufanisi wa kiutendaji.
Zulu Nkanyiso, Meneja Mwandamizi wa Mtambo wa uchenjuaji akijibu maswali kutoka kwa Gillian Doran, Afisa Mkuu wa Fedha wa AngloGold Ashanti, kuhusu muongozo wa GGML wa usimamizi na uhifadhi wa takasumu (TSF). Pia walikuwepo Gilbert Chamlonde, Meneja wa Uchimbaji wa kina kifupi juu ya ardhi (kushoto). Kutoka kulia kwenda kushoto: Yusuph Mhando, Meneja Mazingira; Ikingo Gombo, Meneja Mwandamizi – Masuala ya fedha & Mnyororo wa ugavi na Godvictor Lyimo, Meneja Mwandamizi - Utatuzi wa Migogoro ya Kodi.
Yusuph Mhando, Meneja Mazingira (aliyeupa mgongo kamera), akimfafanulia CFO wa AngloGold Ashanti Gillian Doran (wa pili kutoka kulia) namna kanuni za mazingira zinazotambuliwa na kufuatwa na GGML katika shughuli zake.  Wengine pichani, kutoka kushoto kwenda kulia ni Ashraf Suryaningrat, Meneja Uendeshaji; Zulu Nkanyiso, Meneja Mwandamizi wa Mtambo wa uchenjuaji; Dk. Kiva Mvungi, Meneja Mwandamizi wa HSE; Ikingo Gombo, Meneja Mwandamizi – Masuala ya fedha ba Mnyororo wa ugavi na Godvictor Lyimo, Meneja Mwandamizi - Utatuzi wa Migogoro ya Ushuru.
Gillian Doran, Afisa Mkuu wa Fedha wa AngloGold Ashanti (katikati), pamoja na Himesh Persotam (mwisho kushoto), Makamu wa Rais: Masuala ya Fedha - Afrika, na Jacques Labuschagne, Meneja Mwandamizi wa masuala ya Ushuru Afrika, (wa pili kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja kando ya mgodi wa Nyamulilima na baadhi ya menejiment ya GGML.

****

NA MWANDISHI WETU
Afisa Mkuu wa masuala ya fedha (CFO) kutoka Kampuni ya AngloGold Ashanti inayomiliki Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML), Gillian Doran wiki iliyopita alikaribishwa na kuutembelea mgodi huo uliopo mkoani Geita.

Mbali na Doran pia Meneja Mwandamizi wa Ushuru – Afrika, Jacques Labuschagne na Makamu wa Rais wa masuala ya Fedha – Afrika, Himesh Persotam pia waliitembelea GGML.

Ziara yao haikuwa ya kihistoria tu, kwani ilikuwa ni ziara ya kwanza ya CFO, lakini pia ilitoa maelekezo muhimu kuhusu shughuli za mgodi huo wa dhahabu wa Geita.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post