SERIKALI KUFADHILI MAFUNZO YA TEHAMA KWA WATUMISHI WA UMMA

 


Na Dotto Kwilasa,Dodoma

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari
Serikali imeweka mpango wa ufadhili wa mafunzo ya TEHAMA ya muda mrefu na mfupi
kwa watumishi wa Umma 500 kwenye kozi za kuongeza ujuzi wa Teknolojia . 

Hayo yameelezwa  leo Januari 29,2024 Jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mohamed Khamis Abdulla wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu kuanza  rasmi  maandalizi ya ujenzi wa Chuo cha TEHAMA Dodoma ambacho kitakuwa na uwezo wa kudahili wanafunzi 15,000 kwa mwaka . 

Ameeleza kuwa mahitaji ya awali ya Chuo hicho, yanajumuisha aina ya majengo na 
masomo yatakayo fundishwa yameandaliwa na kuwasilishwa na Exim Bank kwa kushirikiana na Washauri elekezi wa Chuo Kikuu cha Hanyang cha Korea mbapo upembuzi wake yakinifu utachukua miezi sita kukamilika. 

Aidha amesema Wizara hiyo pia imetumia nafasi hiyo kuwatangazia watumishi wa Serikali kuomba ufadhili wa masomo ya muda mrefu na muda mfupi yanayoyolewa na Serikali kuhusu masuala mbalimbali ya TEHAMA. 

"Serikali imeweka mpango wa ufadhili wa mafunzo ya muda mrefu na mfupi
kwa watumishi wa Umma 500 kwenye kozi za kuongeza ujuzi
kwenye masuala yanayohusu Tehama hususani Teknolojia , " amesema

Amefafanua kuwa katika awamu ya kwanza jumla ya watumishi wa umma 20
wameweza kufadhiliwa katika mafunzo ya muda mrefu katika vyuo vikuu nje
ya nchi ambapo kozi walizoenda kuongeza ujuzi ni kwenye masuala
yanayohusu  Teknolojia zinazoibukia.

"Lengo
ni kuwajengea uwezo Maprofesa hao kwenye Teknolojia zinazoibukia na
watakapomaliza waweze kuendelea kutoa mafunzo katika vyuo walivyotoka
na wakati Chuo Mahiri cha Tehama kinaendelea kujengwa, "amesema.

Pamoja hayo ameeleza kuwa nafasi 15 zitatolewa kwa watumishi wa Umma kutoka kwenye Taasisi ya
benki ya Tanzania (BOT) watumishi watano, Mamlaka ya Mapato (TRA )watano, 
Akili bandia kwenye ukusanyaji wa kodi), Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA
Watano kwenye big data analytics pamoja na Akili bandia huku nafasi 10 zitatolewa kwa Watumishi wa Umma kwenda kusoma kwenye
masoma ya Anga za Juu. 

"Tupo kwenye maandalizi ya mwisho ya kupeleka wataalamu 40 kwenye
mafunzo ya muda mrefu nje ya nchi ambapo kati ya hao 15 ni Maprofesa
kutoka Chuo Kikuu cha Dar- es Salaam (5), Chuo Kikuu cha Dodoma (5)
pamoja na Mbeya University of Science and Technology (MUST - 5) ;"amesema

Hivyo basi napenda kuwatangazia watumishi wote wa Serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuwa
tumefungua dirisha la maombi hayo kupitia tovuti ya www.scholarship.go.tz." Amesema
Kwa upande wa timu  ya Washauri elekezi
inaongozwa na Prof. Taejoon Park imesema hatua hiyo imetokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na nchi hiyo na kwamba kazi hiyo itafanywa kwa ufanisi na ujuzi mkubwa kwa kipindi cha muda wa miezi sita.

Amesema, "Ujenzi wa Chuo Mahiri cha Tehama eneo la Nala Dodoma
yameanza rasmi leo tarehe 29 Januari, 2024 na itasaidia kuongeza ufanisi kulingana na mahitaji ya Tehama na kupunguza tatizo la ajira kwa vijana ikiwa ni pamoja na kuendana na mapinduzi ya viwanda Duniani ya mapinduzi ya nne, ya tano na ya sita, "amesema

Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)Profesa Lugano Kusiruka,amesema Chuo hicho kama wadau wa TEHAMA
wamefurahi kushiriki kwenye maandalizi ya ujenzi huo na kwamba utakapo kamilika itasaidia kuwainua vijana wajuzi na kukuza uchumi wa kidigitali kitaifa na kimataifa. 

Amesema Rais Samia ana maono makubwa ya kuwaandaa wananchi kushiriii mapinduzi hayo hivyo UDOM kama wadau wataendeleza maono hayo kwa kusafiri pamoja katika kuijenga Tanzania yenye mapinduzi ya TEHAMA.

"Kwa kuwa na Sisi tuna ndaki ya TEHAMA tutashirikiana bega kwa bega kufanikisha maono ya Serikali kuwatayarisha wataalam watakaofundisha chuo hiki kinachoanza kujengwa ,tayari tumetenga jengo kwa ajili ya jambo hili kuwapika vijana kutafsiri maono ya Rais Samia, lengo ni kuongeza uwekezaji unaoendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia Duniani, "amesisitiza

Ameongeza," Kwa kuwa Serikali yetu inaendelea kuwekeza na Sisi kama wataalamu tutahakikisha tunatimiza wajibu wetu kutoa nafasi kwa wataalam wetu kujiandaa kufundisha chuo hicho, "anasisitiza makamu huyo mkuu wa UDOM.
 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post