TBS YAADHIMISHA WIKI YA UBORA DUNIANI

Mkurugenzi Mkuu (TBS) Dkt. Athuman Ngenya, akifungua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Ubora Duniani mapema leo katika ofisi ya TBS Ubungo, Dar es salaam.

****************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt.Athuman Ngenya amesema wazalishaji na watoa huduma wanahitajika kujengewa au kujijengea utamaduni wa ubora na ushindani hapa nchini na kufahamu uhusiano kati ya ubora na dhana nzima ya ushindani.

Ameyasema hayo leo Novemba 6,2023 Wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Ubora Duniani kwa Mwaka 2023 ambapo amesema moja ya hatua zilizochukuliwa na Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara ili kujenga utamaduni wa kuthamini ubora kwenye jamii yetu ni kuanza kuadhimisha Wiki ya Ubora Duniani

Aidha amesema kuwa Malengo ya kuanzishwa kwa maadhimisho ya wiki ya ubora ni pamoja na kuwaleta karibu wadau wote wa ubora kujadili na kutafakari kwa pamoja masuala yote yanayohusiana na ubora katika nyanja mbalimbali za uchumi na usitawi wa jamii.

"Lengo jingine la kuwa na maadhimisho haya ni kuhamasisha ubunifu na uboreshaji wa bidhaa na huduma zinazotolewa hapa nchini kupitia taratibu zilizowekwa chini ya miundombinu ya ubora". Amesema

Amesema kuwa katika mazingira ya sasa yenye mabadiliko ya mara kwa mara kudumisha nguvu ya ushindani kunahitaji zaidi ya uthabiti wa utendaji.

"Inahitajika kutumia mbinu za uboreshaji wa ubora ili kuendelea kudumu katika ushindani, hivyo niwahimize kuendelea kujifunza mbinu mbalimbali za uboreshaji wa ubora katika utendaji wetu". Amesema Dkt.Ngenya

Pamoja na hayo amesema kuwa iwapo unataka kutoa huduma yenye thamani ya juu zaidi kwa mteja, kufikia malengo na ufanisi wa hali ya juu, lazima ujenge utamadumi wa ubora (Quality Culture) katika kila jambo unalolifanya.

Kauli mbiu ya mwaka huu katika wiki ya ubora ni Quality: realizing your competitive potential. Kauli mbiu hii imekuja wakati muafaka ambapo, Tanzania imedhamiria kuboresha uchumi kupitia sekta ya viwanda na biashara.
Mkurugenzi Mkuu (TBS) Dkt. Athuman Ngenya, akifungua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Ubora Duniani mapema leo katika ofisi ya TBS Ubungo, Dares salaam.
Dkt. Ngenya alisema maadhimisho ya wiki ya ubora vanalenga kuwaleta karibu wadau wote wa ubora kuadili na kutafakari kwa pamoja masuala yote yanayohusiana na bora katika nyanja mbalimbali za uchumi na ustawi wa jamii.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post