TGNP YAPONGEZWA KATIKA HARAKATI ZA KUMKOMBOA MTOTO WA KIKE KIFIKRA


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KATIKA Kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Kike Duniani, Mtandao wa Jinsia Tanzania umekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanatoa mafunzo jinsi ya kuendelea kumlinda mtoto wa kike dhidi ya ukatili kwenye jamii na maeneo mengine yanayomzunguka.

TGNP imekuwa na Kampeni za mara kwa mara kuhakikisha mwanamke anapata haki zake zote za msingi, na miongoni mwa kampeni ambazo wamekuwa wakizifanya ni pamoja na kampeni ya kupinga ukeketaji kwa watoto wa kike, kampeni ambayo ilibeba kauli mbiu "HAKEKETWI MTU ilikuwa ni kipindi ambacho mtoto wa kike anapelekwa kwenye Mila za ukeketaji.

Akizungumza leo Oktoba 11,2023 katika Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS), Mwanaharakati Bi. Zawadi Kondo amesema katika kuhakikisha mwanamke anakombolewa kifikra, wameangazia jitihada mbalimbali katika kuendelea kumlinda mtoto wa kike na kumjengea uwezo katika masuala ya Uongozi.

"Tumeona vitu mbalimbali TGNP wamefanya kama kuanzisha klabu za jinsia mashuleni ambazo zimekuwa chachu katika malezi ya mtoto na vile wanavyo fundishwa na walimu ambao ni walezi wao" ,amesema.

Aidha Bi. Zawadi ameipongeza TGNP katika jitihada zao katika urekebishwaji au Ushauri wa Sera ambazo zinatengenezwa na Jamulhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuhakikisha jamii inaishi kwa usawa na kupata haki zote za msingi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post