TANZANIA YATAJA MAFANIKIO ELIMU KWA WATOTO WA KIKE



Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike yaliyofanyika leo Oktoba 11,2023 katika Shule ya Wasichana Msalato jijini Dodoma.

Na Alex Sonna-DODOMA

SERIKALI imetaja mafanikio sita ambayo Tanzania inajivunia katika sekta ya elimu kwa mtoto wa kike ikiwa ni pamoja na kutekelezwa kwa Waraka wa Elimu namba tatu Mwaka 2021 wa kuwarejesha shuleni wasichana waliokatiza masomo kwa sababu mbalimbali ikiwamo ujauzito ambao hadi sasa 7,995 wamerejea.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda,ameyasema hayo leo Oktoba 11,2023 jijini Dodoma kwenye maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike iliyofanyika Shule ya Wasichana Msalato.

Alisema utekelezaji wa waraka huo ulitokana na maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhimiza mtoto yeyote asiachwe nyuma katika suala la elimu.

““Nina salamu zangu kwa UNICEF naialika ishirikiane na wizara yetu kutoa rasilimali fedha katika kufanya utafiti kwa kufuatilia wale wote ambao wamerudi shule mmoja mmoja kumhoji kuangalia mazingira, mafanikio, changamoto na mapendekezo ya namna bora zaidi ya kutekeleza maelekezo haya ya Rais Samia ya kuhakikisha hakuna mtoto atakayeachwa nyuma kwenye elimu,”amesema.

Aidha, amesema kwa Mwaka 2022/23 wanafunzi 636 waliofaulu vizuri kwenye masomo ya sayansi ikiwamo wanafunzi wa kike 261 ambao ni sawa na asilimia 41 ya wanafunzi wamenifaika na Samia Scholarship.

“Kumekuwapo na mazingira wezeshi kupitia miongozo, miundombinu na vifaa mbalimbali yaliwezesha watoto wenye mahitaji maalum kupata elimu, kila mwaka serikali inatenga fedha ya kununua vifaa,”amesema.

Ametoa wito kwa watoto wenye mahitaji maalum ambao wanahitaji msaada maalum kwa ajili ya kusoma watoe taarifa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Waziri Mkenda pia amesema idadi ya wanafunzi waliodahiliwa katika Taasisi za Elimu ya Juu imeongezeka kwa asilimia 31 kutoka wanafunzi 423,025 ambapo kati yao wa kike ni 177,905 kwa mwaka 2019/20 hadi kufikia wanafunzi 555,166 ambapo kati yao wa kike ni 249,009 kwa mwaka 2022/23.

Kuhusu walionufaika na mikopo ya elimu ya juu, amesema idadi yao imeongezeka kutoka wanafunzi 131,659 kwa mwaka 2019/20 hadi kufikia wanafunzi 202,016 kwa mwaka 2022/23 na ongezeko hili ni sawa na ongezeko la asilimia 53, miongoni mwa wanufaika ni wanafunzi wa kike ni 50,145 kwa mwaka 2019/20 na wanafunzi 85,793 kwa mwaka 2022/23 ongezeko hili ni sawa na asilimia 71.

“Wizara imejenga shule mpya 26 za wasichana ambapo kila mkoa kwa Tanzania bara ni shule moja na shule nyingine moja kwa kila kata kwa watoto wa kike na wakiume ili kupunguza umbali kutoka nyumbani kwenda shuleni jambo ambalo limepunguza changamoto ambazo wangekutana nazo wakati wa kwenda shule,”amesema.

Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, Husna Sekiboko, amesema Bunge na kamati haitakuwa kikwazo katika mipango ya serikali ya kumuendeleza na kumlinda mtoto wa kike nchini.

“Tutahakikisha watoto wa kike wanatimiza ndoto zao na si jambo la kufikiria wewe ni shahidi wabunge walichangishana na kujenga shule ya wasichana ya Bunge kwa lengo la kuionesha serikali na jamii kwamba wabunge wanaunga jitihada za kumlea na kumlinda mtoto wa kike Tanzania,”amesema.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini, Dk.Daniel Baheta, amesema shirika hilo litaendelea kujitolea kuunga mkono jitihada za serikali katika kuwaendeleza wasichana na kuwawezesha.

“Tumeshuhudia serikali ikiondoa vikwazo vinavyokwamisha upatikanaji wa elimu bora kwa wasichana na uamuzi wa kuruhusu wasichana wajawazito, watu wazima na wasichana, mama vijana kurudi shule tunapongeza sana,”amesema.

Mmoja wa wanufaika wa Mradi wa SEQUIP, Neema Chaopa, amemshukuru Rais Samia kwa kuwafuta machozi watoto wa kike kupitia mradi huo ambao wengi wao walikuwa wamekata tamaa baada ya kukatisha masomo yao kwa sababu mbalimbali.

“Kupitia mradi wa SEQUIP tumefutwa machozi tumerejesha ndoto zetu upya wengine tulitamani kuwa waandishi wa habari. Watoto wa kike tumepewa fursa nyingine yakurudisha ndoto zetu.”

“Tunasoma na wengine kutoka mikoa mbalimbali ambao wanasoma kupitia Taasisi ya Watu Wazima kuna mabinti walikuwa wanauza mboga huku wanasoma walipata ujauzito, wengine walishakuwa wafanyakazi wa ndani katika umri mdogo lakini kwa tamko la mama sisi tukarudi shuleni, leo tena tumesimama, tumependeza,”amesema

Awali, Mkurugenzi wa Elimu kutoka Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Susan Nussu, amesema Ofisi hiyo imesimama imara kusimamia viongozi wote kuanzia ngazi za chini kuhakikisha watoto wa kike wanakuwa kwenye mazingira salama.


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike yaliyofanyika leo Oktoba 11,2023 katika Shule ya Wasichana Msalato jijini Dodoma.


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda,akisisitiza jambo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike yaliyofanyika leo Oktoba 11,2023 katika Shule ya Wasichana Msalato jijini Dodoma.


Mkurugenzi wa Elimu kutoka Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Susan Nussu,akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike yaliyofanyika leo Oktoba 11,2023 katika Shule ya Wasichana Msalato jijini Dodoma.


Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini, Dk.Daniel Baheta,akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike yaliyofanyika leo Oktoba 11,2023 katika Shule ya Wasichana Msalato jijini Dodoma.


Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, Husna Sekiboko,akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike yaliyofanyika leo Oktoba 11,2023 katika Shule ya Wasichana Msalato jijini Dodoma.


Wadau mbalimbali wakizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike yaliyofanyika leo Oktoba 11,2023 katika Shule ya Wasichana Msalato jijini Dodoma.


Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda,(hayupo pichani) wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike yaliyofanyika leo Oktoba 11,2023 katika Shule ya Wasichana Msalato jijini Dodoma.


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda,akiangalia igizo kutoka kwa wanafunzi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike yaliyofanyika leo Oktoba 11,2023 katika Shule ya Wasichana Msalato jijini Dodoma.


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike yaliyofanyika leo Oktoba 11,2023 katika Shule ya Wasichana Msalato jijini Dodoma.


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda,akiagana na wanafunzi mara baada ya kuhitimisha kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike yaliyofanyika leo Oktoba 11,2023 katika Shule ya Wasichana Msalato jijini Dodoma.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post