AJALI YA BASI LA FRESTER, LORI NA PIKIPIKI YAUA WATU WAWILI MANYONI


Pikipiki iliyokanyagwa na lori la Tumbaku

Watu wawili wamefariki dunia baada ya kupata ajali wilayani Manyoni mkoani Singida, katika barabara kuu ya Dodoma- Singida eneo la Zimamoto nje kidogo ya mji wa Manyoni, ajali ambayo imehusisha magari matatu ikiwemo basi la kampuni ya Frester lililokuwa likitokea Dar es Salaam.

Mashuhuda wa ajali hiyo iliyotokea Septemba 6,2023 wamesema kuwa watu hao waliokuwa na pikipiki walikuwa nyuma ya basi huku chanzo cha awali cha ajali hiyo kila ikionesha uzembe dereva wa basi kutaka kupita lori lilikuwa limepaki na kusababisha ajali hiyo.

Akithibisha kutokea kupokea vifo hivyo na majeruhi daktari wa zamu katika hospitali ya wilaya Manyoni amesema kuwa walipokea miili ya watu wawili wakiwa wamefariki na majeruhi mmoja ambapo amepatiwa matibabu na kuruhusiwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post