YANGA SC YAICHAPA JKT TANZANIA 5-0, YAJIKITA KILELENI


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KLABU ya Yanga imeendelea kutoa dozi nzito kwenye ligi kuu Tanzania bara maarufu NBCPL mara baada ya kufanikiwa kuizamisha mabao 5-0 Timu ya JKT Tanzania Mchezo uliopigwa kwenye dimba la Chamazi Complex Jijini Dar es Salaam.

Yanga SC walienda mapumziko wakiwa mbele ya bao moja lililofungwa na Stephane Aziz Ki kwa Free kick dakika ya 45 +3 baada ya Musonda kuchezewa rafu karibu na lango kla JKT lililoenda moja kwa moja na kumshinda golikipa wa JKT.

Kipindi cha pili kilikuwa kibaya kwa JKT baada ya kuruhusu nyavu zao kutikiswa mara tatu Yanga SC walipata bao la pili mnamo dakika ya 54 likifungwa na Mshambuliaji Kennedy Musonda akimalizia pasi ya Nickson Kibabage.

Yanga waliendelea kulisakama lango la wapinzani na katika dakika ya 64 beki kitasa kwa sasa kwenye Ligi Kuu Yao Attohoula Kouassi alipiga chuma cha tatu kwa bao safi kwa kuachia shuti kali lililoenda moja kwa moja kwenye Nyavu.

Kipenzi cha wanayanga kijana wa kuchomekea Max Nzengeli alihitimisha safari ya kufunga mabao matano akifunga katika dakika ya 79 na 87.

Kwa ushindi huo Yanga SC wamerudi Kileleni kwa kufikisha Pointi 6 sawa na Azam FC na Simba SC Yanga SC wakiwa na idadi kubwa ya mabao wakifunga mabao 10 na kutoruhusu bao lolote.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post