WAZIRI NDALICHAKO NA KATAMBI WAPONGEZWA KWA KUSHUGHULIKIA MASUALA YA WASTAAFU

 

 WAZIRI  wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako na Naibu Waziri wa Ofisi hiyo, Mhe. Patrobas Katambi wakiwa bungeni wakisikiliza maswali mbalimbali yaliyoulizwa na wabunge kuhusu masuala ya wastaafu leo  Agosti 29, 2023 bungeni Dodoma.

.............

Spika wa Bunge, Mhe. Dkt.Tulia Ackson amempongeza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako na Naibu Waziri wa Ofisi hiyo, Mhe. Patrobas Katambi kwa kushughulikia kwa karibu masuala ya wastaafu.

Dkt.Tulia ametoa pongezi hizo Agosti 29, 2023 bungeni baada ya Naibu Waziri Katambi kujibu maswali ya wabunge kuhusu masuala ya wastaafu.

Amesema “Naibu Waziri ameonesha utayari kama Mbunge ana changamoto apelekewe, mimi ni shahidi wanafanya kazi nzuri Waziri Ndalichako na Naibu Waziri Katambi, wanasikiliza hoja ukiwapelekea na wanafuatilia kuhakikisha mtumishi au mstaafu anasaidiwa.”

Amesema kuna umuhimu wa kuendelea kutoa elimu kuhusu hifadhi ya jamii huku akipongeza maboresho yanayoendelea kufanywa kwenye utoaji huduma kwa wastaafu.

Awali, Naibu Waziri Katambi amesema serikali imekuwa ikishughulikia masuala ya wastaafu kwa kuwasikiliza na kutatua changamoto zao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post