NAIBU WAZIRI MWAKIBETE ATOA PONGEZI KWA CHUO CHA BAHARI

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Atupele Mwakibete akitia saini kwenye kitabu cha wageni alipotembelea banda la DMI

*************

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Atupele Mwakibete (MB), amekipongeza Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kwa kuendelea kutoa mafunzo ya Ubaharia kwa maendeleo ya Uchumi wa Bluu.

Mhe. Mwakibete amesema hayo alipotembelea kwenye banda la Chuo cha Bahari Dar es Salaam kwenye maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya John Mwakangale vilivyopo Jijini Mbeya.

Chuo cha Bahari Dar es Salaam kinashiriki katika maonesho ya Nanenane 2023 jijini Mbeya ambapo huduma mbalimbali zinatolewa katika banda lao zikiwemo kutoa elimu ya ubaharia, elimu ya uokozi wakati wa dharula melini pamoja na usajili kwa wanafunzi wanaohitaji kujiunga na chuo.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Atupele Mwakibete akitoa maelekezo kwa watumishi wa DMI

Watumishi wa DMI wakiendelea kutoa huduma kwa wateja waliotembelea banda la DMI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post