WAZIRI GWAJIMA AZINDUA MRADI WA KUONGEZA USHIRIKI WA WANAWAKE NA WASICHANA KATIKA SEKTA YA USAFIRI NA USAFIRISHAJI “PINK RIDE PROJECT”

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt Dorothy Gwajima akipanda moja ya bajaji alizozindua na kukabidhi katika uzinduzi wa Programu ya Kuchochea Usawa wa Jinsia katika Sekta ya Usafirishaji kupitia mradi wa “Pink Ride: Ndoto yake” iliyofanyika leo Julai 13,2023 katika viwanja vya TGNP Jijini Dar es Salaam.

*************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt Dorothy Gwajima amepongeza Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kuandaa na kuratibu program ya kuwainua wasichana kiuchumi kupitia fursa za ajira katika sekta ambazo zinaaminiwa kuwa za wanaume.

Ametoa Pongezi hizo leo Julai 13,2023 wakati wa Uzinduzi wa Programu ya Kuchochea Usawa wa Jinsia katika Sekta ya Usafirishaji kupitia mradi wa “Pink Ride: Ndoto yake” iliyofanyika katika viwanja vya TGNP Jijini Dar es Salaam.

Amesema sekta ambazo zinaaminiwa kuwa ni za wanaume, ni sekta zinazokuwa kwa kasi na zenye fursa nyingi za ajira na kipato. Mfano wa sekta hizo ni pamoja na sekta ya usafirishaji, TEHAMA, Maliasili na Utalii, Viwanda na Biashara, Ujenzi, Madini na uziduaji na pamoja na nyinginezo.

Aidha amesema mradi huo unatoa fursa za ajira kwa wasichana kama sehemu ya kuendeleza usawa wa jinsia katika sekta ya usafirishaji.

"Leo Wasichana kumi watapewa magari ya matairi matatu (Three Wheelers) kwa ajili ya kwenda kuyatumia kibiashara ili kujipatia kipato. Wasichana hawa wameiva kwani wamepitia mafunzo mbalimbali ya uwezeshwaji kiuchumi kwa takribani mwaka na nusu. Nimeambiwa kuwa hii ni awamu ya kwanza bado kuna wengine wanaandaliwa ambapo baada ya mwaka mmoja, kutakuwa na awamu nyingine katika mikoa mingine nje ya Dar es Salaam". Amesema Waziri Gwajima

Ameeleza kuwa mradi huo ulifadhiliwa na Ubalozi wa Australia ambapo, kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu, wasichana 50 waliweza kufaidika na fursa za mafunzo ya udereva na wasichana 20 waliweza kujifunza uchomeleaji.

"Nimefurahi kusikia kuwa mradi huu ulitoa pia fursa ziadi ambapo baada ya mafunzo awali ya udereva wengine walijiendeleza kujifunza kuendesha magari ya magurudumu matatu, nawengine kuendesha folk lifts na malori". Amesema

Pamoja na hayo amewapongeza Benki ya Maendeleo kwa kuwapatia wasichana hao mikopo yenye masharti nafuu yamkini wasingeweza kupata rasilimali hizo kwa ajili ya kujiajiri.

Vilevile Waziri Gwajima amewapongeza Car & General kwa kutoa magari hayo ya miguu mitatu na kuyafanyia branding pamoja na kutoa mafunzo mbali mbali kwa wasichana hao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TGNP Bi. Gemma Akilimali amesema TGNP kwa kushirikiana na Maendeleo Bank na Car & General, tunaratibu mradi wa kuwainua wasichana kiuchumi na ambapo pamoja na shughuli nyingine ni kuwawezesha washiriki kupata magari ya magurudumu matatu yaani (Three Wheelers) kutoka mkoa wa Dar es Salaam.

"Hii ni sehemu ya kuwawezesha wasichana kuingia kwenye taaluma zinazodhaniwa ni za “wanaume”. Mchakato utawawezesha kupunguza wasichana waliokatika mazingira magumu kujiinua kiuchumi". Amesema

Hata hivyo ametoa rai kwa wanawake, wasichana, na wananchi wote wa Tanzania kuendelea kujiunga na fursa mbalimbali zinazojitokeza kwenye tasnia ya usafirishaji na sekta zingine zinaodhaniwa ni za wanaume.

Amesema kwa upande mwingine, tasnia ya usafirishaji pia ni tasnia yenye changamoto nyingi za kijinsia ikiwemo udhalilishaji na ukatili wa kijinsia, hivyo basi ametoa hamasa kwa jamii kuangalia namna tasnia hiyo inaweza kuwa salama kwa ajili ya makundi yote katika jamii.

"Nitoe Rai pia kwa wanawake wote Tanzania kutokukubali rushwa ya ngono pindi wanapotaka kuajiriwa ili kukwepa fedheha mbalimbali mambo yanapobadilika. Ombi langu pia kwa madereva wa watoto wadogo wachunguzwe kwa umakini ili kuepusha vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto wadogo". Amesema Bi.Gemma

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi.Lilian Liundi amesema Wasichana hao Pink Riders wamepitia changamoto mbali mbali za maisha ndio maana walipewa kipaumbele katika mradi huo.

Amesema Mradi huo pia unatoa fursa kutathmini na kutafakari pengo la kijinsia kwenye tasnia hiyo ya usafirishaji kama takwimu ziavyoonesha kuwa ni asilimia 22 tu ya wafanyakazi wa usafirishaji ni wanawake (takwimu za Ubalozi wa Ulaya (European Commission)
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt Dorothy Gwajima akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Programu ya Kuchochea Usawa wa Jinsia katika Sekta ya Usafirishaji kupitia mradi wa “Pink Ride: Ndoto yake” iliyofanyika leo Julai 13,2023 katika viwanja vya TGNP Jijini Dar es Salaam.Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt Dorothy Gwajima akizungumza katika uzinduzi wa Programu ya Kuchochea Usawa wa Jinsia katika Sekta ya Usafirishaji kupitia mradi wa “Pink Ride: Ndoto yake” iliyofanyika leo Julai 13,2023 katika viwanja vya TGNP Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TGNP Bi. Gemma Akilimali akizungumza katika uzinduzi wa Programu ya Kuchochea Usawa wa Jinsia katika Sekta ya Usafirishaji kupitia mradi wa “Pink Ride: Ndoto yake” iliyofanyika leo Julai 13,2023 katika viwanja vya TGNP Jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi.Lilian Liundi akizungumza katika uzinduzi wa Programu ya Kuchochea Usawa wa Jinsia katika Sekta ya Usafirishaji kupitia mradi wa “Pink Ride: Ndoto yake” iliyofanyika leo Julai 13,2023 katika viwanja vya TGNP Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo PLC, Bw.Ibrahim Mwangalaba akizungumza katika uzinduzi wa Programu ya Kuchochea Usawa wa Jinsia katika Sekta ya Usafirishaji kupitia mradi wa “Pink Ride: Ndoto yake” iliyofanyika leo Julai 13,2023 katika viwanja vya TGNP Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi.Lilian Liundi akizungumza na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt Dorothy Gwajima mara baada ya Waziri huyo kuwasili katika viwanja vya TGNP leo Julai 13,2023 kwenye uzinduzi wa Programu ya Kuchochea Usawa wa Jinsia katika Sekta ya Usafirishaji kupitia mradi wa “Pink Ride: Ndoto yake”
Baadhi ya wadau mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Programu ya Kuchochea Usawa wa Jinsia katika Sekta ya Usafirishaji kupitia mradi wa “Pink Ride: Ndoto yake” iliyofanyika leo Julai 13,2023 katika viwanja vya TGNP Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt Dorothy Gwajima, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi.Lilian Liundi na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo PLC, Bw.Ibrahim Mwangalaba wakiwa kwenye picha ya pamoja na Pink Riders katika uzinduzi wa Programu ya Kuchochea Usawa wa Jinsia katika Sekta ya Usafirishaji kupitia mradi wa “Pink Ride: Ndoto yake” iliyofanyika leo Julai 13,2023 katika viwanja vya TGNP Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments