WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAIBUKA KIDEDEA MAONESHO YA 47 YA SABASABA

Wizara ya Maliasili na Utalii imeibuka Kidedea kwenye Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara (Saba Saba) Jijini Dar es Salaam na kukabidhiwa tuzo na  Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ally  Mwinyi ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika ufungaji wa Maonesho hayo. 


Akielezea Tuzo hiyo ya Banda bora na mashuhuri upande wa Wizara na Taasisi, Mwenyekiti wa Maonesho ya Saba Saba Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Filex John, amesema ni Matokeo chanya ya Uongozi mzuri wa Wizara hiyo pamoja na kazi nzuri iliyofanywa na Watumishi wa Wizara hiyo ya utoaji huduma kwa Kiwango cha juu kwa wote waliofika kwenye Banda hilo. 

Bw. John amewashukuru wadau  na wananchi  wote waliojitokeza kupata huduma kwenye Banda hilo la Maliasili, pamoja na ushirikiano waliotoa katika kuhakikisha Maonesho hayo yanakuwa na Mafanikio Makubwa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post