AJALI YA LORI NA HIACE YA KAHAMA - NGARA YAUA WATU SITA RUNZEWE


Watu sita wamefariki dunia na wawili kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha  gari dogo la  abiria aina ya Toyota Hiace yenye namba za usajili T766 DQP ambayo imegongona   na roli la mizigo lenye Namba D9954A ( SCANIA) katika Eneo la Runzewe  wilayani Bukombe.

Akizungumzia kuhusu ajali hiyo Kamanda wa Jeshi la  Polisi Mkoa wa Geita,  ACP  Safia Jongo amesema  ajali imetokea leo  Julai 13 majira ya saa kumi na moja alfarji ambapo gari la abiria lilikuwa likitokea Kahama kwenda Ngara huku Lori lilikuwa likisafiri kutoka Rwanda kuelekea Nairobi nchini Kenya.

Amesema chanzo cha ajali hio ni uzembe wa dereva la gari la abiria ambaye inadaiwa alikuwa ananzinzia  kitendo ambacho kilipelekea kuhama upande wake na kwenda kuparamia lori.

"Dereva wa Lori alifanya huhudi kubwa kulikwepa ila ikashindikana na kusababusha ajali hiyo" amesema Jongo 

Amesema majeruhi Hali zao ni Mbaya wamelewa kituo Cha Afya cha Uyovu na Sasa wamehamishwa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Geita.

Ameeleza, ajali imetokea leo  Julai 13,  majira ya saa 05:00 alfajiri eneo la kata ya Runzewe ambapo gari dogo ilikuwa ikitokea Kahama kwenda Ngara huku lori likisafiri kutoka Rwanda kuelekea Nairobi.

Jongo amesema uchunguzi wa awali unaonyesha chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari dogo,, Habibo bedi ambaye anadaiwa alisinzia, kisha kuacha njia yake na kwenda upande wa pili wa lori.

"Dereva wa roli alifanya juhudi kukwepa, lakini dereva wa Hiace alikuwa kwenye mwendo kasi hivo kusababisha ajali hiyo iliyopelekea vifo vya watu sita akiwemo dereva wa ‘Hiace’ na kondakta wake." Kamanda Jongo.

“Majeruhi hali zao ni mbaya, walikuwa kituo cha afya cha Uyovu, na sasa hivi wamehamishiwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Geita, hali zao haziendelei vizuri ila wanaongea na  nimeweza kuongea nao.”Kamanda Jongo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post