MKURUGENZI SALU SECURITY BANDORA SALUMU MIRAMBO AZINDUA ALBAM YA MSHINDI WA YOTE ,KWAYA YA NVC NGOKOLO KANISA LA AIC SHINYANGA


Mkurugenzi wa kampuni ya Salu Security Bandora Salum Mirambo akizindua albam ya Mshindi wa yote kwaya ya Ngokolo Vijana Choir (NVC) katika kanisa la AIC Ngokolo Manispaa ya Shinyanga


Na Mwandishi wetu


Mkurugenzi wa kampuni ya Salu Security Bandora Salum Mirambo ameongoza uzinduzi wa albam ya Mshindi wa yote kwaya ya Ngokolo Vijana Choir (NVC) katika kanisa la AIC Ngokolo Manispaa ya Shinyanga huku akichangisha fedha kwa ajili ya kuunga mkono kwaya hiyo .


Akizungumza na waumini wa kanisa la AICT Ngokolo Manispaa ya Shinyanga 
leo Jumapili Julai 16,2023  Bandora amewashukuru waumini wa Kanisa la AIC Ngokolo Shinyanga kwa kuendelea kumkumbuka na kumshirikisha katika shughuli za kijamii hususani za kanisa huku akinukuu kitabu kitakatifu biblia Mithali 8: 17-21, amemshukuru Mungu kwa neema zake na kwa upendo mkubwa kwa taifa letu.


Bandora amewaomba waumini na wakristo kumuombea mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, “Tumuombee mama yetu na Rais wetu maisha marefu na afya njema azidi kutuongoza kwa hekima na busara, pia naomba waumini muendelee kuliombea taifa amani, utulivu na upendo".


Pia Bandora amewasihi wazazi na walezi kuimarisha malezi ya watoto wao ikiwa ni pamoja na kushirikiana na serikali kukemea vitendo vya ukatili na mmomonyoko wa maadili hali itakayosaidia kuwa na kizazi chenye hofu ya Mungu katika jamii huku akiwataka vijana wa kanisa hilo kufanya kazi ili kujiletea maendeleo na kuepuka kufanya matendo yasiyofaa .


Kwa upande wake Katibu wa kwaya ya NgokoloVijana Choir (NVC ) Gaspary Elias akisoma risala ya kwaya hiyo mbele ya mgeni Rasmi ameeleza kuwa kwaya hiyo inakabiliwa na changamoto ya ununuzi wa vyombo vya muziki licha ya kwaya hiyo kufanikiwa kizindua Albam yenye nyimbo nane ambazo zitasambazwa katika maeneo mbalimbali ya Shinyanga na nje ya Shinyanga kwa lengo la kuhubiri na kulitangaza neno la Mungu.
Mkurugenzi wa kampuni ya Salu Security Bandora Salum Mirambo akipokea risala.
Burudani zinaendelea.

Mkurugenzi wa kampuni ya Salu Security Bandora Salum Mirambo akijiandaa kuzindua albam ya wimbo wa Mshindi wa yote kwaya ya Ngokolo Vijana Choir (NVC) katika kanisa la AIC Ngokolo Manispaa ya Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments