TBS KUTUMIA MAONESHO YA SABASABA KUWAFIKIA WAJASIRIAMALI WADOGO


KATIKA kuelekea msimu wa SABASABA, Shirika ka Viwango Tanzania (TBS) litatumia maonesho hayo kuwafikia wajasiriamali wadogo ikiwa ni pamoja na kuwatembelea kwenye maeneo yao na kuwahudumia.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo Juni 26,2023 Jijini Dar es Salaam, Meneja wa Uhusiano na Masoko TBS, Bi.Gladness Kaseka amesema katika Maonesho ya mwaka huu watawatembelea wajasiriamali kujua changamoto zao hususani kwa wale ambao hawajapata alama ya ubora kwani huduma hiyo TBS huwa wanatoa bure.

"Zoezi hili litakuwa linalenga kuhakikisha kwamba wajasiriamali wanapata alama ya ubora ya TBS". Amesema Bi.Gladness.

Aidha amesema kupitia maonesho hayo watakuwa na madawati mbalimbali ikiwemo dawati la huduma la usajili wa majengo ya bidhaa za chakula na vipodozi.

"Kwa wale ambao watataka kusajili majengo yao ya chakula na vipodozi, huduma hii wataipata hapo kwa papo katika msimu huu wa sabasaba". Amesema

Pamoja na hayo Kaseka amewakaribisha wadau wote kutembelea banda la TBS ili kupata taarifa mbalimbali ikiwemo na kupokea maoni malalamiko na hata kuzitatua papo kwa hapo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post