ASKOFU BUGOTA AFUNGUA SEMINA YA IDARA YA WANAWAKE WAKANISA LA AICT ,AWAPA JUKUMU LA KUKEMEA MMOMONYOKO WA MAADILI.


Askofu wakanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga Askofu Zakayo Bugota akifungua Semina ya wanawake kutoka dayosisi 7 za kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT )


Washiriki wa Semina kutoka Dayosisi saba za kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT ).

NA MWANDISHI WETU MALUNDE  BLOG 

Makamu wa Askofu Mkuu wa AICT Askofu Zakayo Bugota ambaye pia ni Askofu wa kanisa la Africa Inland Church Tanzania, Dayosisi ya Shinyanga leo amefungua semina ya idara ya wanawake wa kanisa la AICT ambayo itafanyika kwa siku tatu katika ukumbi wa chuo cha ualimu SHYCOM mjini Shinyanga.

 

Askofu Bugota ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha kuendelea kushirikiana na serikali pamoja na wadau wengine katika juhudi za kukemea mmomonyoko wa maadili, tabia na destori kandamizi pamoja na migogoro ya ndoa na familia.

 

Askofu Bugota Amesema kuwa ipo haja ya wanawake wakanisa hilo kuendelea kushirikiana ili kuhakikisha wanapaza sauti ya pamoja kukemea tabia zinazokwenda kinyume na maadili ikiwemo mavazi yasiyo na staha.


Ipo changamoto ya ndoa za masafa ambazo nindoa unakuta mwanaume anafanya kazi mkoa tofauti na mkoa anapo fanyia kazi mwenza wake hili ni tatizo ambalo kwa kiasi kikubswa linachangia migogoro katika familia. 

 

“changamoto kama hii ya ndoa za masafa inahitaji mkakati wa pamoja utakao saidia kupunguza changamoto hiyo katika jamii yetu”.

 

“Kuna migogoro ya ndoa na familia hii ni mojawapo ya chanzo cha ongezeko la watoto wa mitaani na hata mauaji ya kutisha tunayoyaona katika jamii na kundi kubwa la waathirika ni wanawake na watoto, pia zipo tabia na desturi kandamizi tuendelee kuelimisha kanisa ili waumi wetu wawe mstari wa mbele katika mabadiliko haya”.amesema Askofu Bugota.

 

Askofu Bugota ametumia nafasi hiyo kuwaomba wanawake hao kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza ikiwemo zile za kiuchumi ili kupata vyanzo vya mapato vitakavyowawezesha kujikwamua kimaisha.

 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa idara ya wanawake kanisa la AICT Martha Misoji amemshukuru Askofu Bugota ambapo ameahidi kuwa idara hiyo itaendelea na jitihada mbalimbali za kuwaimarisha wanawake wa kanisa hili.

Amesema Dayosisi zinazoshiriki semina hiyo ni Dayosisi ya Pwani, Dayosisi ya Mwanza, Dayosisi ya Geita, Mara, ukelewe pamoja na Dayosisi ya kati.

 

Naye Mwenyekiti wa CCT  Naila Mayala ametumia nafasi hiyo kuwasisitiza washiriki wa semina hiyo kuwa mabalozi wazuri kwa wengine.

Aidha  Naila amewaomba wanawake hao kuendelea kushirikiana katika kutokomeza Mmomonyoko wa maadili na kutoa elimu juu ya malezi na makuzi ya watoto.

 

Wanawake wa kanisa la AICT katika Dayosisi saba leo Jumatano Juni 14,2023 wameanza semina ya siku tatu yenye lengo la kuwaimarisha kimwili na kiroho kukemea mambo maovu ikiwa ni maandalizi ya kuelekea wiki ya wanawake inayofanyika kila Mwaka mwezi Septemba.

 

Askofu wakanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga Askofu Zakayo Bugota akifungua Semina ya wanawake kutoka dayosisi 7 za kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT )Matha Misojii mwenyekiti wa idara ya wanawake kanisa la AICT Tanzania akizungumza na washiriki wa semina.

Askofu Zakayo Bugota askofu wa dayosisi ya Shinyanga akiwa na askofu wa dayosisi ya Tabora Askofu Joshua Lusato.


Askofu Zakayo Bugota askofu wa dayosisi ya Shinyanga akiwa na askofu wa dayosisi ya Tabora Askofu Joshua Lusato na msaidizi wa askofu Bugota mchungaji Charles Lugembe wakiwa katika picha ya pamoja.


                Naila Mayara Mwenyekiti CCT Tanzania 


Washiriki wa Semina kutoka Dayosisi saba za kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT ).
Washiriki wa Semina kutoka Dayosisi saba za kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT ).

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post