WANAJAMII WAELEZA MARAJIO CHANYA KATIKA BAJETI KUU YA NCHI KUHUSU MUELEKEO WA HALI YA UCHUMI 2023/2024


NA EMMANUEL MBATILO

WANAJAMII katika Semina za Jinsia na maendeleo (GDSS) wamekutana na kueleza matarajio yao katika bajeti kuu ya nchi kuhusu muelekeo wa hali ya uchumi kuelekea mwaka 2023-2024 na kusikiliza mgawanyo wa Bajeti katika mlengo wa Kijinsia ambapo wanatarajia kuona utekelezaji wa yale ambayo hayakutekelezwa katika bajeti iliyopita.

Bajeti Kuu ya Nchi inatarajiwa kuwasilishwa hapo kesho Juni 15,2023 Bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Mwigulu Nchemba.

Akizungumza wakati wa majadiliano hayo, Mwezeshaji wa Semina za Jinsia na maendeleo (GDSS) Bw. Jophrey Chambua amesema kwenye sekta ya kilimo wanatarajia kuona mabadiliko kuanzia kwenye masuala ya pembejeo na mengineyo ili kuona nchi inaondokana na changamoto za njaa na chakula na hatimae kila mtu aweze kunufaika na kilimo.

Katika sekta ya Elimu, Bw.Chambua amesema kumekuwa na jitihada nyingi za kuboresha miundombinu ya elimu ambayo imesaidia kuongezeka kwa ufaulu nchini, hivyo basi tutarajie kuona miundombinu inaboreshwa zaidi katika maeneo mbalimbali hasa vijijini.

"Tunatarajis kusikia miundombinu inaongezeka kwa upande wa ujenzi wa mabweni ya wasichana lakini pia kuhakikisha kunakuwa na uwiano wa matundu ya vyoo pamoja na uwiano wa vitabu vya kusomea". Amesema Bw.Chambua

Kwa upande wa wanajamii wamesema wanatarajia kuona miundombinu ya maji hasa kutokana na uchakavu wa mabomba, miundombinu kuwa hafifu, wanatarajia maboresho yatafanyika na maji kupatikana kwa wingi kwenye maeneo mbalimbali nchini.

"Tunatarajia kusikia Serikali inatuambia upatikanaji wa maji kwa wingi vijijini na mijini na taifa kuondokana na uhaba wa maji ya kutosha". Amesema Bw. Miraji Simba

Nae Bi.Jamila Kisinga amesema kutokana na wanawake kuwa na changamoto mbalimbali hasa pale wanapokuwa katika hedhi, Serikali iangalie ni namna gani wanaweza kuboresha maeneo maalumu ya kujistiri wasichana mashuleni pindi wanapokuwa katika hedhi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post