AFARIKI KWA KUKANYAGWA NA LORI AKIIBA MUWA ..."GARI LILIKUWA SPIDI KALI"Mwanaume mmoja mwenye umri wa makamo ameaga dunia baada ya kukanyagwa na trela/Lori lilokuwa likisafirisha miwa kwenye barabara ya Kachok kuelekea Kondele nchini Kenya.

Kwa mujibu wa kamanda wa trafiki ukanda wa Nyanza Joseph Ng'ang'a, mwanaume huyo alikuwa akijaribu kuvuta kipande cha muwa kutoka kwa trela hilo lililokuwa likienda kwa kasi. 

Ng'ang'a anasema kuwa mwanaume huyo alivutwa kwa nguvu na trela hilo na magurudumu ya nyuma kumkanyaga hadi kufariki papo hapo. Visa vya watu kuvuta miwa kutoka kwa trela, malori na matingatinga eneo la Nyanza na Magharibi ni vya kawaida.

Mara nyingi wanaohusika katika visa hivi husubiri malori haya kando ya barabara na kuvuta miwa kutoka kwao kisha kuanza kuitafuna. 

Ng'ang'a anasema kuwa trela hilo ambalo lilikuwa likielekea katika kiwanda cha Kabras katika uliokuwa mkoa wa Magharibi limepelekwa katika kituo cha polisi cha Kondele kwa ukaguzi.

 Dereva wa trela hilo hakupata jeraha lolote huku mwili wa mwendazake ukipelekwa katika hifadhi ya maiti ya Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga jijini Kisumu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post