ESTER APATIKANA, ALICHUKULIWA NA MUUZA MKAA


Kushoto ni mwanafunzi Ester na kulia ni Mama yake mzazi


Mwanafunzi Ester Noah Mwanyilu, amepatikana katika chumba cha kupanga cha Mama Abdul kilichopo maeneo ya Ifisi Mbalizi, na kwamba alipelekwa hapo na muuza mkaa aitwaye Baba Jose na kusema ni mke wake hivyo anaomba hifadhi baada ya siku mbili angemchukua ili wakaishi wote.

Aidha vipimo vyote vya kiafya vimefanyika na Ester hana ujauzito na hivyo ataendelea kukaa na maafisa ustawi wa jamii ili kumsaidia kumpa ushauri wa kisaikolojia arudi shule, na mwanaume huyo atasakwa mpaka akamatwe.

RC Homera ametoa rai kwa walimu wa Pandahill kupunguza kasi ya kuchapa viboko.

Jana Juni 22, 2023, Waziri Mkuu alitoa maagizo kuhakikisha mwanafunzi huyo anapatikana mara moja na baadaye Juni 23, 2023, Mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Homera alitoa saa 24 na kutangaza dau la milioni 5 kwa yeyote atakayefanikisha kumpata mwanafunzi huyo.

Mwanafunzi Ester Noah Mwanyilu, alipotea kwenye mazingira ya kutatanisha akiwa shuleni kwao Pandahill Mei 18 mwaka huu.

CHANZO - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post