DAWA YA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME MAARUFU AKAYABAGU, VUMBI LA KONGO ZAPIGWA MARUFUKU

Dawa inayoongeza nguvu za kiume maarufu 'Akayabagu' pamoja na vumbi la Kongo zimepigwa marufuku kutumika kwa kile kilichoelezwa kuwa hazijathibitishwa ubora wake.

Hayo yamesemwa jana Ijumaa, Juni 23, 2023 na Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Profesa Hamis Malebo kupitia taarifa kwa umma.

"Baraza limepata taarifa ya uwepo wa dawa asili inayotumika kama kinywaji na jamii kubwa hasa wanaume ijulikanayo kwa jina la Akayabagu, hivyo liliamua kufanya uchunguzi wa uingizwaji, usambazwaji, ubora na usalama wa kinywaji hicho," amesema.

Profesa Malebo amesema kinywaji hicho ambacho kinadaiwa kuongeza nguvu za kiume, kimechanganywa na dawa ya kisasa aina ya Sildenafil (Viagra majina mengine Erecto ama Vega) jambo ambalo ni kinyume cha Sheria.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post