SERIKALI YAZINDUA MIONGOZO YA ELIMU YA AWALI

Mkurugenzi Msaidizi Ithibati Shule, Bw. Patrick Leyana,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Miongozo ya Elimu ya Awali kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda hafla iliyofanyika katika Shule ya Msingi Mtemi Mazengo jijini Dodoma.Kushoto ni Mkurugenzi wa Elimu ya Awali na Msingi kutoka Ofisi ya Rais, TAMISEMI,Bi.Susan Nussu.

Na Alex Sonna-DODOMA

SERIKALI imezindua miongozo na nyaraka za Elimu ya Awali zitakazorahisisha utoaji wa huduma stahiki kwa watoto kwenye malezi na ujifunzaji ili kujenga makuzi timilifu.


Uzinduzi huo umefanyika Mei 26, 2023 na Mkurugenzi Msaidizi Ithibati Shule, Patrick Leyana kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda katika Shule ya Msingi Mtemi Mazengo jijini Dodoma.

Amesema miongozo na nyaraka hizo zimeandaliwa ili kuwawezesha wadau wa elimu ya awali kutoa huduma kwa watoto wote kwa usawa na kwa kuzingatia mahitaji yao.

Ametaja miongozo hiyo kuwa ni pamoja na Mwongozo wa Kitaifa wa Uendeshaji na Viwango katika Elimu ya Awali (MUVEA), Kiongozi cha Utekelezaji wa Mwongozo wa Kitaifa wa Uendeshaji na Viwango katika Elimu ya Awali (KUMUVEA), Mwongozo wa Kitaifa wa Uanzishaji na Utekelezaji wa Shughuli za Ushirikiano wa Wazazi na Walimu katika Elimu ya Awali na Msingi.

Mingine ni Mwongozo wa Kitaifa wa Uanzishaji, Usimamizi na Uendeshaji wa Vituo Shikizi vya Shule pamoja na Mwongozo wa Upimaji Shirikishi wa Matokeo ya Ujifunzaji kwa Wathibiti Ubora wa Shule.

“Shukrani za pekee kwa Shirika la Kimataifa la Watoto Duniani UNICEF na GPE LANES II pamoja na mashirika mengine likiwemo shikrika la Children in Crossfire Watoto wetu Tunu Yetu, USAID- Jifunze Uelewe na UKaid-Shule Bora mliochangia kwa moyo wa dhati kufanikisha uandaaji, uchapaji na uzinduzi wa miongozo hii,”amesema.

Amewaomba viongozi wengine kutoka katika wizara zinazohusika na masuala ya watoto kutumia miongozo hiyo ili kuwezesha upatikanaji wa huduma jumuishi kwa watoto wote wakiwemo wenye mahitaji maalumu kufikia viwango vya ubora wa kitaifa, kikanda na kimataifa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Elimu ya Awali na Msingi kutoka Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Bi.Susan Nussu, amesema miongozo hiyo itasaidia kujenga elimu bora kwa watoto wa kitanzania wakiwa na umri mdogo na kupitia mradi wa BOOST walimu 3,000 watafikiwa kujengewa uwezo wa kufundisha madarasa ya awali.

Awali Mratibu wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Hawa Selemani, amesema miongozo hiyo itaweka viwango vya ubora katika utekelezaji wa elimu ya awali.

Naye Mtaalamu wa masuala ya Elimu kutoka Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Audax Tibubinda, amesema hatua hiyo inaonesha hatua kubwa katika maendeleo ya elimu na kuhimiza wataalamu wa ndani waendelee kutumika zaidi ili kuleta mafanikio ya aina hiyo.



Mkurugenzi Msaidizi Ithibati Shule,Bw. Patrick Leyana,akizungumza wakati akifungua uzinduzi wa Miongozo ya Elimu ya Awali Tanzania bara kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda hafla iliyofanyika katika Shule ya Msingi Mtemi Mazengo jijini Dodoma.


Mkurugenzi wa Elimu ya Awali na Msingi kutoka Ofisi ya Rais, TAMISEMI,Bi.Susan Nussu,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Miongozo ya Elimu ya Awali Tanzania bara hafla iliyofanyika katika Shule ya Msingi Mtemi Mazengo jijini Dodoma.


Mratibu wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Hawa Selemani,akielezea malengo ya uzinduzi huo wa Miongozo ya Elimu ya Awali Tanzania bara hafla iliyofanyika katika Shule ya Msingi Mtemi Mazengo jijini Dodoma.



Mtaalamu wa masuala ya Elimu kutoka Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Audax Tibubinda,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Miongozo ya Elimu ya Awali Tanzania bara hafla iliyofanyika katika Shule ya Msingi Mtemi Mazengo jijini Dodoma.


Mkuu wa Divisheni ya Elimu ya Awali kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bw.Hamd Habib Bakar,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Miongozo ya Elimu ya Awali hafla iliyofanyika katika Shule ya Msingi Mtemi Mazengo jijini Dodoma.


Mkufunzi Mhonda TC Bw.Mussa Swila,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Miongozo ya Elimu ya Awali Tanzania bara hafla iliyofanyika katika Shule ya Msingi Mtemi Mazengo jijini Dodoma.


Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii,JinsiaWanawake na Makundi Maalum Bi.Leah Mwakatobe,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Miongozo ya Elimu ya Awali Tanzania bara hafla iliyofanyika katika Shule ya Msingi Mtemi Mazengo jijini Dodoma.

Mratibu wa Elimu ya Awali Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt.Yangson Mgogo,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Miongozo ya Elimu ya Awali Tanzania bara hafla iliyofanyika katika Shule ya Msingi Mtemi Mazengo jijini Dodoma.


Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi Ithibati Shule,Bw. Patrick Leyana (hayupo pichani), wakati akifungua uzinduzi wa Miongozo ya Elimu ya Awali Tanzania bara kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda hafla iliyofanyika katika Shule ya Msingi Mtemi Mazengo jijini Dodoma.


Mkurugenzi Msaidizi Ithibati Shule,Bw. Patrick Leyana,akipata maelezo jinsi watoto wanavyopata elimu ya awali wakati wa uzinduzi wa Miongozo ya Elimu ya Awali Tanzania bara kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda hafla iliyofanyika katika Shule ya Msingi Mtemi Mazengo jijini Dodoma.


Mkurugenzi Msaidizi Ithibati Shule,Bw. Patrick Leyana,akicheza na watoto wakati akifungua uzinduzi wa Miongozo ya Elimu ya Awali Tanzania bara kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda hafla iliyofanyika katika Shule ya Msingi Mtemi Mazengo jijini Dodoma.


Mkurugenzi Msaidizi Ithibati Shule,Bw. Patrick Leyana,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Miongozo ya Elimu ya Awali kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda hafla iliyofanyika katika Shule ya Msingi Mtemi Mazengo jijini Dodoma.Kushoto ni Mkurugenzi wa Elimu ya Awali na Msingi kutoka Ofisi ya Rais, TAMISEMI,Bi.Susan Nussu.

Mkurugenzi Msaidizi Ithibati Shule,Bw. Patrick Leyana,akikabidhi Miongozo ya Elimu ya Awali mara baada ya kuizindua kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda hafla iliyofanyika katika Shule ya Msingi Mtemi Mazengo jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi Ithibati Shule,Bw. Patrick Leyana,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua Miongozo ya Elimu ya Awali Tanzania bara kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda hafla iliyofanyika katika Shule ya Msingi Mtemi Mazengo jijini Dodoma.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments