AJIKATA UUME AFE AKISEMA AMECHOKA KUUMWA MUDA MREFU



Mkazi wa Kijiji cha Kibitilo kata ya Ilula Wilayani Kwimba mkoani Mwanza Marco Samweli (32) amelazwa katika hospitali ya Rufaa ya kanda Bugando baada ya kujikata nyeti zake kwa kutumia kisu na kisha kuzitupa kwa madai ya kuwa amechoka kuumwa ugonjwa uliokuwa ukimsumbua kwa miaka mitatu.


Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa amesema tukio hilo limetokea mara baada ya mwanaume huyo kutoka hospitali kwa kwaajili ya matibabu ya maradhi yanayomsumbua na kueleza kuwa amekata tamaa ya kupona na kuamua kujikata uume wake.

Aidha kamanda Mutafungwa amesema kwa sasa mgonjwa huyo anapatiwa matibabu akiwa chini ya ulinzi wa jeshi hilo kutokana na kitendo alichofanya cha kujijeruhi na pindi atakapopona jeraha lake atafikishwa mahakamani kujibu shtaka linalomkabili.

Chanzo- EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post