AJIUA BAADA KUUA WATU NANE



“Tulianza kukimbia, watoto walikuwa wakikanyagwa”. Anaeleza Maxwell Gum (16),mfanyakazi wa stendi karibu na eneo ambalo mauaji ya risasi ya watu nane katika jiji la Texas Marekani . Yeye na wengine walijihifadhi kwenye chumba cha kuhifadhia vitu.

Mauaji haya yametekelezwa na mtu mmoja aliyekuwa na bunduki ambapo alifyatua risasi kwenye jumba la maduka eneo la Dallas na kujeruhi saba kabla ya kuuawa na afisa wa polisi ambaye alikuwa karibu kulingana na taarifa ya mamlaka.

Polisi hawakutoa maelezo mara moja kuhusu wahanga wa tukio katika eneo la Allen Premium Outlets, kituo kikubwa cha maduka ya nje, lakini mashuhuda wameripoti kuwaona watoto miongoni mwao. Wengine wamesema pia waliona afisa wa polisi na mlinzi wa maduka wakiwa wamepoteza fahamu.

Picha za video za kamera iliyopachikwa kwenye gari zilisambaa mtandaoni kuonesha mshambuliaji huyo akishuka kwenye gari na kuwafyatulia risasi watu waliokuwa kando ya barabara. Zaidi ya risasi dazeni tatu zilisikika wakati gari lililokuwa likirekodi picha hizo likiondoka.

Takriban watu saba wanatibiwa hospitalini, watatu kati yao ni wakiwa mahututi. Mkuu wa Zimamoto Allen Jonathan Boyd amesema watu saba ikiwa ni pamoja na mshambuliaji huyo walitangazwa kufariki katika eneo la tukio na wawili walifariki baadaye hospitalini.

Gavana wa Republican wa Texas Greg Abbott ambaye ametia saini sheria za kupunguza vikwazo vya umiliki wa bunduki kufuatia ufyatuaji risasi wa watu wengi hapo awali aliita ufyatuaji risasi wa maduka hayo "janga lisiloelezeka".

Ufyatuaji risasi Texas ni tukio la hivi punde zaidi wa kile ambacho kimekuwa kasi kubwa ya mauaji ya watu wengi nchini Marekani. Wiki moja kabla, mtu mmoja aliwaua kwa kuwapiga risasi watu tano huko Cleveland, Texas baada ya jirani yake kumwomba kuacha kufyatua risasi wakati mtoto amelala.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post