WAZIRI WA KAZI CHARLES ENGOLA AUAWA KWA KUPIGWA RISASI


Waziri wa Kazi, Ajira na Uhusiano wa Viwanda Nchini Uganda, Charles Okello Engola ameuawa leo asubuhi kwa kupigwa risasi na Mlinzi wake (Bodyguard), Spika wa Bunge la Uganda Anitha Among amethibitisha Bungeni leo Jumanne Mei 2,2023.

Tukio hilo limetokea leo asubuhi ambapo imeripotiwa kuwa Waziri Okello alikuwa anatoka nyumbani kwenda kazini ambapo ghafla Mlinzi wake alimpiga risasi kisha akaanza kupiga risasi juu huku akikimbiakimbia Mtaani.

Majirani wamesema Mlinzi huyo alisikika akisema hajalipwa mshahara kwa muda mrefu licha ya kufanya kazi na Waziri huyo.

Inaripotiwa kuwa Mlinzi huyo baadaye aliingia Saluni moja iliyopo Jirani na nyumba ya Waziri kisha akawataka waliokuwa ndani kutoka nje na akajifungia na kujipiga risasi na kufariki pia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments