JAMAA AJICHIMBIA KABURI KISHA KUPANDA MAUA PEMBENI


Nicholas Ireri kutoka katika kijiji cha Nguruka kaunti ya Embu amewaacha wengi vinywa wazi baada ya kujichimbia kaburi kutokana na kile kinachokisiwa kuwa mzozo wa familia.


Mwanamme huyo mwenye umri wa 52 na ameripotiwa kutumia siku nzima kulichimba kaburi lake na kisha kupanda maua eneo la kaburi hilo.

Ireri anasemekana kuhofia maisha yake kwa madai kuwa kuna jamaa zake wa karibu ambao walipanga kumvamia na kumnyang'anya kipande chake cha ardhi. 

Naibu chifu wa eneo hilo Esther Nyaga amewataka wakaazi kutafuta njia mbadala ya kusuluhisha matatizo ambayo yanawakumba.

"Nilipata ujumbe huo na kweli nilipoendea katika eneo hilo nilipata tayari Nicholus Ireri akiwa amelichimba kaburi. Nawasihi wakaazi kutojiingiza katika malumbano yanayoweza kusababisha maafa na badala yake kufanya mazungumzo yatakayo hakikisha kuwepo kwa amani," Nyaga alieleza. 

Wenyeji walipomsihi Ireri kuacha kuchimba kaburi hilo anasemekana kupandwa na hasira na kuwaonya dhidi ya kumfahamisha mke wake na watoto wake kuhusu yaliyokuwa yakijiri.

"Kuanzia sasa hivi nataka kuwaonya familia yangu dhidi ya kuwapigia mke na watoto wangu. Tafadhali familia yangu achaneni na mimi. Naomba mwenyezi Mungu anisadie niweze kupata maridhiano kati yangu, dadaangu, kaka yangu na wajomba zangu. Kwa sasa familia yangu iniache niishi maisha yangu," Ireri alisema.

 Kinachosubiriwa ni kuona iwapo mzozo wa shamba kati ya Ireri na familia yake utatatuliwa ili amani irejee kati ya jamaa hawa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post