TAHARUKI MTI ULIOANGUSHWA NA UPEPO KISHA KUKATWA KATWA WAINUKA NA KUWA KIVUTIO


Wakazi wa kijiji cha Kambiri nchini Kenya wameachwa vinywa wazi baada ya mti uliokatwa na kuanguka chini kupatikana umesimama tena imara.

Kwa mujibu wa ripoti ya K24 Digital, wakazi wanasema mti huo uliangamizwa miaka miwili iliyopita lakini sasa umeibuka tena shambani.

Ni kisa ambacho kimegeuka kuwa fumbo na sasa wakazi wamekuwa wakifika eneo tukio kushuhudia maajabu hayo. 

Kevin Mbalilwa aliambia ripota kuwa mti huo uliangushwa na upepo mkali miaka miwili iliyopita na hata kuvunjwa kuni.

Hata hivyo, katika hali ambayo bado haijaeleweka, mti huo sasa umesimama imara shambani na wakazi hawaamini macho yao.

 Mwenye shamba hilo amewataka maafisa wa Wizara ya Misitu kufika eneo hilo angalau kujaribu kutatua hali.

 "Ninataka maafisa wa mambo ya misitu kufika hapa ili waniambie vile ninaweza kunufaika na kisa hiki. Watu wamekuwa wakifika eneo hili kuona kisa hiki na hawanipatii lolote ila kuharibu mahindi yangu," alisema.

Mkulima huyo anataka sasa mti huo kugeuzwa na kuwa kivutio kwa watalii akisema shamba lake linapokea wageni kila siku kuona maajabu hayo. 

"Ninaomba maafisa wa KFS wakuje na wafanye huu mti kuwa kivutio cha watalii ili nipate kitu," alisema kwa wanahabari. 

Baadhi ya wakazi hata hivyo wanasema hawawezi kufika eneo hilo kamwe wakihofia kuwa huenda kilichotokea ni mwiko. Wanasema ni lazima familia husika kuita wazee ili matambiko yanayofaa yafanywe na kugeuza hali.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments