KIWANDA CHA CHOKOLETI CHAUA WATU WATATU


Idadi ya watu waliofariki kutokana na mlipuko katika kiwanda cha chokoleti uliotokea jimboni Pennsylvania nchini Marekani, Ijumaa, Machi 24,2023 imeongezeka na kufikia watu watatu.

Watu wanne pia wanaripotiwa kutoweka kufuatia tukio hilo huku maafisa wa eneo hilo wakisema shughuli za uokoaji zinaendelea kuwatafuta manusura. 

Maafisa wa usalama bado walikuwa wakiondoa vifusi kufuatia mlipuko huo wa Ijumaa alasiri katika kiwanda cha RM Palmer Company katika eneo la West Reading, Pennsylvania. 

Hata hivyo, kutokana na ghasia za mlipuko na muda ambao umepita, nafasi ya kupata manusura inapungua kwa kasi.

Mkuu wa Idara ya Wazimamoto wa West Reading, Chad Mayor aliwaambia waandishi wa habari Jumamosi, Machi 25, 2023 kuwa kutokana na ghasia za mlipuko na muda ambao umepita, nafasi ya kupata manusura inapungua kwa kasi.

Picha za tukio hilo zilionyesha moto ukiwaka kwenye vifusi baada ya mlipuko huo, huku wazima moto wakijaribu kuuzima. "Kiwanda kimesawazishwa sana, kwa bahati mbaya. 

Hakuna mengi wanayoweza kuokoa kutoka kwa jengo hilo," Meya wa West Reading Samantha Kaag aliwambia waandishi wa habari. 

"Mbele, na kanisa na vyumba, mlipuko ulikuwa mkubwa kiasi kwamba ulisogeza jengo la futi nne mbele," aliongeza. 

Mkuu wa Polisi wa West Reading Wayne Holben naye aliongeza akisema: "Mwili wa tatu ulikuwa katika eneo la RM Palmer na umethibitishwa kuwa marehemu." 

"Wahudumu wanaendelea na juhudi zao za kupekua vifusi ili kupata watu wengine wengine," Holben alisema. Kwa sasa watu wanne hawajulikani waliko kufuatia mkasa huo ambao bado chanzo chake kinachunguzwa na mamlaka.

Kampuni ya RM Palmer imekuwa ikitengeneza chokoleti ainati ya msimu kama vile Pasaka na peremende za Siku ya Wapendanao zenye umbo la moyo tangu mwaka wa 1948.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post