MKE AMUUA MMEWE KWA KUMKATA SEHEMU ZA SIRI


Msemaji wa polisi nchini Uganda Fred Enanga akizungumza na wanahabari Jijini Kampala nchini Uganda

**
Polisi mjini Kampala nchini Uganda wanamshikilia mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Joy Biira kwa tuhuma za kumkata mumewe sehemu za siri jambo lililosababisha kifo cha mwanaume huyo.


Msemaji wa polisi nchini Uganda Fred Enanga amesema mwanamke huyo mkazi wa Tarafa ya Makindye jijini Kampala anatuhumiwa kusababisha kifo cha Benson Baluku ambaye alikuwa akiishi naye kama mume

Kwa mujibu wa polisi, marehemu alirejea nyumbani Machi 26 akiwa amelewa na kuanza kupigana na mkewe ambaye kila mara alimtuhumu kuwa na mahusiano ya nje ya ndoa.

Polisi wamesema mume alimshika mkewe shingoni na kuanza kumnyonga hali iliyomfanya mke atoe kisu na kumkata sehemu za siri.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post