MADIWANI SHINYANGA WAKASIRISHWA VITENDO VYA KINYAMA WANAVYOFANYIWA WATOTO... "KESI ZISHUGHULIKIWE KIKAMILIFU, KIMYA KIMYA INAUMIZA"

Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye Kikao cha Baraza.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MADIWANI wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wametoa tamko la kulaani vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto wadogo vinavyoendelea ndani ya jamii, yakiwamo matukio ya ubakaji na ulawiti.

Wametoa tamko hilo leo Februari 10, 2023 kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wakati akichangia Taarifa ya Kamati ya Uchumi, Afya na Elimu.

Wamesema matukio ya ukatili dhidi ya watoto katika Manispaa ya Shinyanga yamekithiri, hivyo elimu inapaswa kuendelea kutolea kwa wananchi kuachana na vitendo hivyo ili kutowaathiri watoto kisaikolojia na kushindwa kutimiza ndoto zao.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Uchumi Afya na Elimu Shela Mshandete, amesema inaumiza sana kuona watoto wadogo wakiendelea kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia, tena wakifanyiwa na watu ambao ni wa karibu.

“Tushikamane madiwani na kutoa Tamko la kulaani matukio ya ukatili dhidi ya watoto wadogo, na ajenda hii ya kupinga ukatili iwe ya kudumu tuzungumza kwenye mikutano yetu yote ikiwamo ya hadhara ili Shinyanga kusiwepo na ukatili tena,”amesema Shela.

“Tunaliomba pia Jeshi la Polisi kesi za ukatili zikifika kwenye dawati lao wazishughulikie kikamilifu ili wahusika wachukuliwe hatua kali za kisheria, na siyo kuzisuluhisha kimya kimya,”ameongeza.

Ametoa wito pia kwa wananchi kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake, ili kuhakikisha watoto wanalindwa dhidi ya vitendo vya ukatili wasome na kutimiza ndoto zao.

Katika hatua nyingine amesisitiza suala la watoto kula chakula shuleni na kuwaomba wazazi wachangie chakula kila mmoja debe moja la unga na kilo 4 za sukari, ambapo mwanafunzi atakula mwaka mzima, na kusoma bila ya kuwa na njaa na hatimaye kufanya vizuri kitaaluma.

Aidha katika Baraza hilo ziliwasilishwa taarifa za Kamati ikiwamo Kamati ya Ukimwi, Kamati ya fedha na Utawala, na Kamati ya Uchumi Afya na Elimu, na kujadiliwa mambo mbalimbali ikiwamo upungufu wa matundu ya vyoo shuleni.

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, akiwasilisha taarifa yake kwenye Baraza hilo, amesema changamoto zote ambazo zimewasilishwa watazifayika kazi na zingine zipo kwenye utekelezaji, huku akisisitiza kwamba hali ya mwenendo ya utendaji katika halmashauri inazidi kuimarika kutoka na kuwepo kwa uwazi na uwajibikaji.

Amesema Halmashauri hiyo itaendelea na kasi ya ukusanyaji wa mapato ya ndani, fedha ambazo zitatumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi.

Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Ester Makune akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura akizungumza kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi Afya na Elimu Shela Mshandete akizungumza kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani.

Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye Kikao cha Baraza.

Kikao cha Baraza la Madiwani kikiendelea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments