MAMA ALIYETESEKA NA UGONJWA USIOJULIKANA AFARIKI AKIFANYIWA MAOMBI KANISANI

Polisi nchini Uganda wanachunguza kisa ambapo mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 59 Rosette Najjuma -ameaga dunia akiwa kanisani jijini Kampala.

Kwa mujibu wa naibu msemaji wa polisi wa Kampala Luke Owoyesigyire, Najjuma alizirai na kufariki ibada ikiendelea katika kanisa la Christian Life katika Parokia ya Makerere III mnamo Jumatano - Februari 8,2023. 

Mwanamke huyo anaripotiwa kufanyiwa vipimo kadhaa katika Hospitali ya Mulago kwa muda wa miaka mitatu iliyopita lakini hakuna ugonjwa uliopatikana.

 Jamaa zake waliamua kumtafutia msaada wa kanisani na hivyo kumpeleka katika kanisa la Pasta Jackson Ssenyonga.

Mwanamke huyo alizirai akifanyiwa maombi mwendo wa saa kumi alfajiri na kuaga dunia kabla ya kufanyiwa msaada wowote wa kimatibabu.

 Owoyesigyire alisema kuwa mwili wake ulihamishiwa makafani ya Mulago ukisubiri kufanyiwa upasuaji.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post