MA DC WAPYA WAAPISHWA SHINYANGA, RC NAWANDA AONYA WAKUU WA WILAYA KUGOMBANA NA WATUMISHI, ATOA MTIHANI WA KWANZA

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga (kulia) Dk. Yahaya Nawanda akimkabidhi vitendea kazi Mkuu wa wilaya mpya wa Kahama Mboni Mhita mara baada ya kumaliza kumuapisha.
Uapisho wa Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Yahaya Nawanda, amewapa mtihani wakuu wa wilaya mkoani humo, hadi kufika siku ya Jumatatu wahakikishe wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza wawe wamesharipoti shule.

Nawanda ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, amebainisha hayo leo Februari 1, 2023 kwenye hafla ya kumuapisha Mkuu wa wilaya mpya wa Kahama Mboni Mhita, ambaye aliteuliwa hivi karibuni na Rais Samia Suluhu Hassan, kuchukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa wilaya hiyo Festo Kiswaga.

Amesema mtihani wa kwanza ambao wanawapa wakuu wa wilaya wapya mkoani Shinyanga akiwamo na Mwenyeji Joseph Mkude wa Kishapu, kuwa wakafanye kazi ya kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza wanaripoti shule, bila ya kujali wana sare za shule au hakuna wote waanze masomo.

“Hadi kufikia siku ya Jumatatu nataka wakuu wa wilaya wote wa Shinyanga mnipatie taarifa kuwa wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza wapo shuleni na huu ndiyo utakuwa mtihani wenu wa kwanza,”amesema Nawanda.

“Kafanye hiyo kazi kwa kushirikiana na Maofisa Elimu, Wakuu wa Polisi wilaya, Maofisa Tarafa na Wakurugenzi na hakuna kiongozi yeyote kutoka nje ya Mkoa hadi watoto wote waripoti shule,”ameongeza.

Amesema Rais Samia ametoa fedha nyingi katika Sekta ya Elimu ikiwamo kuboresha miundombinu ili watoto wapate elimu na kutimiza ndoto zao, hivyo wao kama wasaidizi wake wanapaswa kusimamia watoto wote wanapata elimu na Taifa hapo baadae kuja kupata viongozi na wataalamu.

Amewataka pia wakuu hao wa wilaya wasiende kugombana na watumishi, bali waende wakafanye kazi kwa ushirikiano pamoja na kugusa maisha ya wananchi kwa kusikiliza kero zao na kuzitatua ikiwamo na migogoro ya ardhi.

“Msiende kuwa watu wa maofisini kakagueni miradi ya maendeleo na kuisimamia, na mtende haki kwa wananchi ili kuhakikisha wilaya zenu pia zinakuwa salama,”amesema Nawanda.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anord Makombe, ametoa wito kwa Wakuu wa Wilaya mkoani Shinyanga, wakafanye kazi kwa ushirikiano na watendaji wote wa Serikali pamoja na kushughulikia malalamiko ya wananchi na kutatua kero zilizopo.

Naye Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita, ameshukuru Rais Samia kwa kumteua kuwa Mkuu wa wilaya hiyo, huku akiahidi kuitumikia nafasi hiyo vizuri kwa ajili ya maslahi mapana ya Taifa.

Mkuu wa wilaya mpya wa Shinyanga Johari Samizi ambaye yeye hakuapishwa ikiwa amehamishwa kutoka wilaya ya Kwimba, alisema hatakuwa mtu wa Ofisi bali atakuwa wa kwenda site kusikiliza na kutatua kero za wananchi, huku akiomba ushirikiano kwa viongozi.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Yahaya Nawanda akizungumza mara baada ya kumaliza kumuapisha Mkuu wa wilaya Mpya wa Kahama Mboni Mhita.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Prof; Siza Tumbo akizungumza kwenye Uapisho wa Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Anord Makombe akizungumza kwenye Uapisho wa Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita.

Mkuu wa wilaya Mpya wa Kahama Mboni Mhita akizungumza mara baada ya kumaliza kuapishwa.

Mkuu wa wilaya mpya wa Shinyanga Johari Samizi ambaye amehamishiwa kazi kutoka wilaya ya Kwimba akizungumza kwenye Uapisho wa Mkuu wa wilaya mpya wa Kahama Mboni Mhita.
Mkuu wa wilaya mpya ya Kahama mkoani Shinyanga Mboni Mhita akila kiapo leo Februari 1, 2023 kuitumikia nafasi hiyo mara baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuwa Mkuu wa wilaya ya Kahama kuchukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa wilaya hiyo Festo Kiswaga.
Mkuu wa wilaya mpya ya Kahama mkoani Shinyanga Mboni Mhita akila kiapo leo Februari1, 2023 kuitumikia nafasi hiyo mara baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Mkuu wa wilaya ya Kahama kuchukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa wilaya hiyo Festo Kiswaga.

Zoezi la ushuhudiaji uapisho wa Mkuu wa wilaya mpya wa Kahama Mboni Mhita likiendelea.

Zoezi la ushuhudiaji uapisho wa Mkuu wa wilaya mpya wa Kahama Mboni Mhita likiendelea.

Mkuu wa wilaya Kishapu Joseph Mkude (kushoto) akiwa na Mkuu wa wilaya mpya wa Shinyanga Johari Samizi, na Mkuu wa wilaya mpya wa Kahama Mboni Mhita.

Mkuu wa wilaya Kishapu Joseph Mkude (kushoto) akiwa na Mkuu wa wilaya mpya wa Shinyanga Johari Samizi, kwenye uapisho wa Mkuu wa wilaya mpya wa Kahama Mboni Mhita.

Mkuu wa wilaya mpya wa Kahama Mboni Mhita.

Zoezi la ushuhudiaji uapisho wa Mkuu wa wilaya mpya wa Kahama Mboni Mhita likiendelea.

Zoezi la ushuhudiaji uapisho wa Mkuu wa wilaya mpya wa Kahama Mboni Mhita likiendelea.

Zoezi la ushuhudiaji uapisho wa Mkuu wa wilaya mpya wa Kahama Mboni Mhita likiendelea.

Mkuu wa wilaya mpya wa Shinyanga Johari Samizi akiwa na Mkuu wa wilaya mpya wa Kahama Mboni Mhita.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, akiwa na Mkuu wa wilaya mpya wa Shinyanga Johari Samizi.

Zoezi la ushuhudiaji uapisho wa Mkuu wa wilaya mpya wa Kahama Mboni Mhita likiendelea.

Zoezi la ushuhudiaji uapisho wa Mkuu wa wilaya mpya wa Kahama Mboni Mhita likiendelea.

Zoezi la ushuhudiaji uapisho wa Mkuu wa wilaya mpya wa Kahama Mboni Mhita likiendelea.

Mkurungezi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, akiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Nice Munissy.

Picha ya Pamoja ikipigwa mara baada ya zoezi la uapisho wa Mkuu wa wilaya mpya wa Kahama Mboni Mhita kumalizika.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments