JAJI MGEYEKWA AWAITA WANANCHI KUJIFUNZA USULUHISHI MIGOGORO YA ARDHI


**************************

Katika kuadhimisha wiki ya sheria, Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi imeandaa siku moja ya kutoa elimu na kukutana na wadaawa katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam siku ya Alhamisi Januari, 26, 2023.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi Mhe. Agnes Mgeyekwa amesema siku hiyo Majaji wa Mahakama yake watakuwepo katika viwanja hivyo kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi.

Amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kujifunza faida za usuluhishi katika masuala mazima ya utatuzi wa migogoro ya ardhi.

Kwa mujibu wa Mgeyekwa, Majaji wa Mahakama hiyo watakuwemo katika Banda hilo la Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi kuanzia saa 3 asubuhi hadi 9 alasiri ambapo watatoa elimu na kukutana na wadaawa.

"Ninawaomba wananchi wajitokeze kwa ajili ya kujifunza faida za usuluhishi katika utatuzi wa migogoro ya ardhi". Alisema Jaji Mgeyekwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments