AFANDE NKALANGO AKAMATWA NA POLISI WENZAKE SIMIYU TUHUMA ZA KUMFANYIA MBAYA MTOTO WAKE


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu Blasius Chatanda.


Na Mwandishi Wetu Simiyu.

Siku moja baada ya blog ya Simiyupressblog kutoa taarifa za mtoto (7) kufanyiwa vitendo vya ukatili na Baba yake anayedaiwa kuwa ni askari wa jeshi la Polisi Bariadi Mkoani Simiyu.


Hatimaye Jeshi la Polisi Mkoani hapa, limejitokeza mbele ya waandishi wa Habari na kuzungumza tukio la mtoto huyo (jina linahifadhiwa) ambaye alipigwa hadi kujeruhiwa na Baba yake anayedaiwa kuwa Askari Polisi kituo cha Polisi Bariadi.

Kamanda wa Polisi Mkoani humo Blasius Chatanda amesema kuwa ni kweli Baba wa mtoto aliyefanya ukatili huo ni Askari wa jeshi hilo, katika kituo cha Polisi Bariadi na anashikiliwa jeshi hilo.


Kamanda Chatanda amesema kuwa wanamshikilia Askari huyo mwenye namba PC H.4178, Abati Benedicto Nkalango (27) kwa kosa la kumpiga mtoto wake na kumsababishia vidonda sehemu mbalimbali za mwili.


Chatanda amesema kuwa askari huyo alimpiga mtoto wake wakati akikagia madaftari ya Shule.


"Mnamo tarehe 15/1/2023,.Majira ya saa 11:00 huko katika kambi ya Kituo Cha Polisi Wilaya ya Bariadi, Askari wa Jeshi la Polisi namba PC H.4178 Abati Benedicto Nkalango (27), msukuma, alimshambulia mtoto wake mwenye umri wa miaka 7 mwanafunzi wa Shule ya msingi Gappa kwa kumpiga na fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia majeraha makubwa", amesema Chatanda.


CHANZO - SIMIYU PRESS CLUB BLOG

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

Post a Comment

Previous Post Next Post