CHONGOLO AKEMEA VIONGOZI WALALAMISHI,ATAKA WATIMIZE MAJUKUMU YAO

 


Na Dotto Kwilasa,Malunde 1 Blog-DODOMA.

CHAMA cha mapinduzi (CCM) kimefanya hafla fupi ya kuwapokea wajumbe wapya wa Sekretarieti  ya chama hicho Jijini Dodoma huku kikiwataka kuhakikisha wanafanya kazi kwa nia na kutatua matatizo ya watanzania na kujibu hoja.

Wajumbe hao wa Sekretarieti mpya ya chama hicho wakiongozwa na Daniel Chongolo-Katibu Mkuu wa CCM ni pamoja na Anamiringi Macha-Naibu Katibu Mkuu CCM Bara,Mohamed Said Mohamed-Naibu Katibu Mkuu Zanzibar,Sophia Mjema-Katibu wa Nec Idara ya Itikadi na uenezi na Dkt.Frank Hawassi-Katibu wa Nec Idara ya Uchumi na Fedha .

Wengine ni Mbarouk Nassor Mbarouk-Katibu wa Nec,Idara ya siasa na uhusiano wa kimataifa (SUKI) na Issa Haji Ussi(Gavu)-Katibu wa Nec Idara ya oganaizesheni.

Akiongea kwenye hafla hiyo,Katibu Mkuu wa Chama hicho Daniel Chongolo ametumia nafasi hiyo kukemea tabia ya baadhi ya viongozi  kuendekeza malalamiko badala ya kufanya kazi kwa kutimiza majukumu yao.

Mbali na kuwakemea Viongozi hao, Chongolo pia amewatangazia amekerwa na viongozi  ambao wanatumia muda mwingi kulalamika na  kueleza kuwa kulalamika kwao kunaonesha wazi kuwa hawatoshi na kama hawawezi kufanya kazi wakae pembeni kuwapisha wanaoweza.

"Changamoto kubwa tuliyonayo ndani ya CCM ni kuwepo kwa baadhi ya watumishi ndani ya serikali kuendelea kulalamika,unamkuta waziri aliyepewa dhamana ya kutimiza wajibu wake,Mkuu wa Mkoa na mkuu wa Wilaya badala ya kutimiza wajibu wao bado wao wanaendekekeza kulalamika.

"Hii ni aibu mfano unawakuta watumishi wa serikali wanaenda kwenye vyomba vya habari wanawalalamikia watendaji waliopo chini yao kuwa hawasaidie kufanya kazi kwa kitendo hicho kinaonesha wazi kuwa hautoshi ni sawa na katibu mkuu kuwalalamikia waliopo chini yake kuwa hawasaidii kazi je unawezaje kulalamika wakati unatakiwa kutumia mamlaka uliyo nayo"amesema 

Katika hatua nyingine Chongolo amesema kuwa Wiki hii wanaanza ziara mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kukagua miradi kuanzia ngazi ya shina huku akiwataka watendaji wa juu wakihakikisha wanatoa ushirikiano na watumishi wa ngazi ya chini.

Aidha Chongolo amesema kuwa kumekuwepo na changamoto ya kuchekeana na kufimbiana macho katika mambo ya msingi ambayo yanagusa maisha ya watu.

Kwa upande wake Katibu wa itikadi na uenezi  wa hicho ,Sophia Mjema amesema kuwa kwa nafasi aliyopewa anaenda kufanyakazi kwa mitazamo tofauti kwani kabla ya kwenda kwa wananchi laxima idara hiyo uelimishajibuwe sawa .

"Lazima mabalozi wetu wakajue wananchi wanataka nini lazima ndugu zetu  tutakapokwenda kwa wananchi tutaenda mpaka ngazi za vitongoji tukajue wananchi wanataka nini,"amesema Mjema.

Amesema katika kukitangaza chama wanaccm wanatakiwa kufanyakazi  wote kwa pamoja kwani hakuna mwingine atakae kilinda chama bali ni wao.

"Nataka tukumbushane tu na wanaccm mwenyekiti wetu lazima tumtetee iwe usiku iwe mchana kazi yetu ni chama cha mapinduzi hivyo lazima tumtete Mwenyekiti wetu.

Ndugu zangu wakina baba na wakinamama, wasichana na wavulana nataka nisikie kwa mioyo yenu mkiimba chama cha mapinduzi,hivyo ndivulyo tutakavyoona maonao ya Mwenyekiti wetu atakayotuletea.

"Subiri muone mnakuja kuona chama chenu kinavyokuja kuwatetea kama kulikua na maonevu tunaenda kuyamaliza kama kuna kero tunaenda kuzimaliza ila tunakuja kwa kutoa alimu ambayo kila mtu atatambua jinsi ya kuelimishana,"amesema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments