MCHUNGAJI WA KANISA LA KKKT ASIMAMISHWA KAZI


Mchungaji Rev. Dr. Eliona Kimaro.

Mchungaji Rev. Dr. Eliona Kimaro wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Usharika wa Kijitonyama, ni miongoni mwa wachungaji wa kanisa hilo wanaofahamika zaidi. Kanisa la Kijitonyama, ni miongoni mwa makanisa makubwa, watu wa madhehebu mbalimbali wakienda kusali hapo katika ibada zake za jioni, Jumapili na nyingine.
.
Jana, Mchungaji Kimaro akiwa katikati ya semina aliyotarajia kuiongoza kwa wiki mbili, aliwaaga washarika wa Kijitonyama na kusema kwamba amepewa likizo ya siku 60, na ameelezwa kwamba baada ya likizo hiyo hatarudi Kijitonyama.
.
Video hii ya wakati Mchungaji Kimaro anaaga, imesambaa katika kurasa mbalimbali na kuibua maoni tofauti, baadhi ya watu wakihusisha jambo hilo na migogoro ambayo imekuwa ikitokea katika Kanisa hilo na wakipinga Kimaro kuondolewa Kijitonyama.
.
Hata hivyo Mchungaji Kimaro hajaeleza sababu za maamuzi hayo ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments