MSANII AMBER LULU ALALAMIKA KUPIGWA SANA ....ATISHIWA KUUAWA


Amber Lulu; ni staa wa muziki wa Kizazi Kipya nchini Tanzania ambaye kwa mara nyingine ameeleza kunyanyaswa au kufanyiwa ukatili wa kipigo.
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Amber Lulu

Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Amber ambaye ni mama wa mtoto mmoja wa kike aitwaye Ariana aliyezaa na msanii Bosheni ameelea kuumizwa vibaya kwa kipigo katika mwili wake.

Kwa mujibu wa Amber Lulu, chanzo kikubwa cha kipigo hicho ni mtoto wake huyo bila kufafanua.
Ameandika; “Daa nimekuwa mtu wa kuhangaika na kuteseka pasipo sababu ya msingi, mapenzi niliyinayo kwa mtoto wangu na uchungu na uvumilivu, Mungu pekee ndiye anajua.
“Kuna muda najitoa nafanya chochote kwa ajili ya mwanangu na nilizaa kwa mapenzi na mapenzi ya Mungu naona ila ninachofanyiwa kama sina haki kuna muda natamani kumkumbatia mwanangu nishinde naye nashindwa cos nisipohangaika mtoto wangu atakula nini? Nyumba nalipa mimi, leo napigwa kama mbwa kisa kumhangaikia mwanangu, naumia sasa hivi mtu anatishia kuniua.“Mpaka naogopa kurudi nyumbani kwangu, mtoto wangu namuita hoteli, ukiangalia mwili wangu kama daah…”
Si mara ya kwanza kwa Amber Lulu kulalamika kupigwa na mwanaume, lakini amekuwa hachukui hatua yoyote dhidi ya ukatili huo wa kijinsia.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

Post a Comment

Previous Post Next Post