MAMLAKA YA DAWA YARUHUSU DAWA ZA KUTOA MIMBA ZIUZWE MTAANI



Kwa mara ya kwanza maduka ya dawa ya rejareja nchini Marekani yanaweza kuuza vidonge vya kutoa mimba, chini ya mabadiliko ya sheria mpya na utawala wa Biden.
Wagonjwa wanaweza kupata vidonge vya kutoa mimba(mifepristone) - ambayo ni salama na yenye ufanisi katika kutoa mimba kutoka kwa mtoa huduma wa afya.


Maelezo ya matumizi bado yanahitajika chini ya sheria mpya, lakini wagonjwa sasa wanaweza kuchukua vidonge hivyo dukani au kutumiwa kwa njia ya barua.


Hatua hiyo inaweza kuongeza kasi ya utoaji mimba kwa kutumia dawa.


Vidonge vya kutoa mimba vimekuwa vikitafutwa zaidi kufuatia uamuzi wa Mahakama ya Juu wa mwaka jana uliobatilisha haki ya shirikisho ya kutoa mimba, huku mataifa kadhaa yakipiga marufuku au kuzuia vikali upatikanaji wa utoaji mimba.


Zaidi ya nusu ya utoaji mimba nchini Marekani tayari unafanywa kwa tembe badala ya upasuaji, kulingana na Taasisi ya Guttmacher inayounga mkono.


Mwezi Disemba mwaka 2021, Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani (FDA) ilisema itaondoa kabisa hitaji la wagonjwa kupata dawa kibinafsi kupitia mtoa huduma ya afya, kama sehemu ya hatua yake inayotokana na janga.


Siku ya Jumanne, FDA ilitoa taarifa mpya katika tovuti yake na mahitaji mapya, ikisema dawa hiyo "inaweza kutolewa na maduka ya dawa yaliyoidhinishwa au chini ya usimamizi wa daktari aliyeidhinishwa".


Danco Laboratories na GenBioPro, kampuni mbili za Marekani zinazotengeneza dawa hiyo, zilithibitisha kwa taarifa tofauti kwamba wakala huo ulikuwa umewafahamisha kuhusu uamuzi wake.


Hatua hiyo imesifiwa kama "hatua muhimu" mbele na Chuo cha Madaktari wa uzazi cha Marekani na Madaktari wa Magonjwa ya Wanawake.

CHANZO - BBC SWAHILI



Je Utoaji mimba/ kutoa mimba ni dhambi?..Je kama mtoto aliye tumboni anahatarisha uhai wa mama na madakatari wakamwambia anapaswa atoe hiyo mimba ili aishi vinginevyo atakufa..je endapo akiitoa ili kunusuru uhai wake kwa sababu za kiafya atakuwa amefanya dhambi ni muuaji?

JIBU: Kwanza ni muhimu kufahamu maana ya utoaji mimba..Utoaji mimba ni kitendo cha mzazi wa kike..kuondoa kiumbe ambacho tayari kimeshaanza kuishi katika tumbo lake..Hicho kinaweza kuwa katika wiki ya kwanza au katika mwezi wa mwisho wa 9. Hatua yoyote inayohusisha kukiondoa hicho kiumbe tumboni kwa mwanamke katika kipindi hicho cha muda ni kitendo cha UTOAJI MIMBA.

Utoaji mimba umegawanyika katika sehemu mbili..1) Utoaji mimba kwa sababu za kiafya 2) Utoaji kwa sababu nyingine zisizo za kiafya.

Tukianza na sababu za kiafya

Hii inahusisha pale mama mjamzito..labda kaugua ghafla na ile mimba ndani ya tumbo lake ikaharibika au mtoto akafa tumboni…Ili kuokoa maisha ya mama analazimika kwenda kuiondoa hiyo mimba hospitalini..Katika hali kama hiyo mama huyo hafanyi dhambi kwasababu tayari mtoto kashakufa..hivyo anapaswa atolewe huko aliko na kuzikwa.

Pia Inaweza kutokea mimba ya mama mjamzito ikatoka yenyewe kabla ya wakati wake…Hali kama hiyo pia hakuna dhambi iliyotendeka..Ingawa sio kawaida mimba kutoka yenyewe…

Lakini pia inaweza kutokea Mama mjamzito kapata tatizo au ugonjwa ambao utamlazimisha aondoe ile mimba iliyopo tumboni mwake ili kunusuru uhai wake. Na asipofanya hivyo kuna hatari ya kufa. Katika hali kama hiyo ambayo imethibitishwa..endapo mimba hiyo akiitoa hafanyi dhambi. Kwasababu amefanya hivyo ili kunusuru uhai wake…na asipofanya yeye pamoja na hicho kiumbe tumboni watakufa.

Lakini pia ni muhimu kufahamu kuwa..Hata katika hali hiyo ambayo madaktari wamesema kwamba ni ngumu kunusuru uhai wa mama akiwa na kiumbe tumboni..YESU KRISTO wa Nazareti hashindwi jambo..Mimba inaweza isitolewe na mwanamke huyo akazaa vizuri kabisa bila kufa wala kupata tatizo lolote..wanadamu wanashindwa mambo lakini Yesu Kristo hana rekodi ya kushindwa…Na wapo wanawake wengi wametendewa na Yesu miujiza kama hiyo…wamepewa ripoti na madaktari kwamba aidha waiondoe mimba waishi au waendelee kukaa na hiyo mimba wafe…lakini Bwana amewapigania na wameshinda vitisho vya vifo na wamejifungua salama kabisa bila tatizo lolote…Na waliotendewa hivyo na Yesu wapo wengi sana.

Lakini hiyo inahitaji imani thabiti isiyo na mashaka kwa Yesu Kristo…Lakini kama mtu ataingiwa na mashaka basi ni heri akaenda kuiondoa hospitalini…Kwasababu biblia imesema mtu asiye na imani asitegemee kupokea kitu kutoka kwa Mungu…


Yakobo 1.6 “… Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.

7 Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.

8 Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote.”

Sababu za PILI za kutoa mimba ni sababu zisizo za kiafya

Sababu hizi zinahusisha…Pale mwanamke anapopata mimba na wakati hana mpango wa kuwa na mtoto kwa wakati huo…Mwanamke wa namna hiyo akiitoa mimba ambayo tayari kashaipata anafanya dhambi..ni Muuaji.

Mwanamke ambaye amepata mimba kwa kubakwa au kwa mtu asiyempenda na akaenda kuitoa anafanya dhambi tayari, ni muuaji.

Mwanamke ambaye kapata mimba na kalazimishwa na mtu aliyempa mimba kwamba aitoe na yeye akaitoa anafanya dhambi huyo ni muuaji kabisa.

Mwanamke ambaye kapata ujauzito na Baba aliyehusika na ujauzito huo kaikataa hiyo mimba na mwanamke akaenda kuitoa hiyo mimba anafanya dhambi ni muuaji.

Mwanamke anayetoa mimba kwasababu ya umasikini au hali ngumu ya kimaisha kwa kuhofia malezi ya mtoto yatakuwaje anafanya dhambi ni muuaji.

Na sababu nyingine zote zilizosalia zisizo za kiafya..Ni dhambi kutoa mimba kwa kutumia hizo sababu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments