ATUPWA JELA MIAKA 30 KWA KUMBAKA BINTI WA KIDATO CHA PILI


Jacob Okafyulilo, mwenye umri wa miaka 38, Mbena na Mkazi wa Kijiji cha Itambo wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe, amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na kuamriwa kulipa fidia ya shilingi milioni moja baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka binti wa kidato cha pili.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi imeeleza kuwa hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mhomi J. E Januari 10, 2023 baada ya mahakama hiyo kujiridhisha pasi na shaka na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri uliothibitisha kuwa, mtuhumiwa alitenda kosa la kumbaka binti wa miaka 16 wa kidato cha pili tarehe 10 Oktoba 2022.

Mwendesha mashtaka wa Serikali Kamwela, aliiomba mahakama itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwa mtuhumiwa ambaye ni mjomba wa mhanga na wengine wenye mawazo ya kutenda uhalifu wa kikatili kama huo.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

Post a Comment

Previous Post Next Post