MAJAMBAZI WAUA MZEE WA MIAKA 90 AKITOKA BENKI


Mzee wa miaka 90 kutoka Kibwezi, Kaunti ya Makueni siku ya Jumanne, Januari 10,2023 aliuawa kinyama na majambazi.

Kwa mujibu wa ripoti ya Citizen Digital, mzee huyo alivamiwa na watu wasiojulikana alipotoka kwenye benki katika eneo la Metava.

Mzee huyo alikuwa ametoka katika benki hiyo, kuchukua pesa zake alizopokea za mpango wa Inua Jamii.

Chifu wa eneo hilo Nicolas Mwonga alithibitisha kisa hicho, akisema majambazi hao walimkata koo mzee huyo na kumuibia pesa zake.

Mwili wa mwendazake umepelekewa katika chumba cha kuhifadhi maiti kwenye Hospitali ya Kambu.

Polisi wameanzisha msako wa kuwanasa washukiwa ambao hadi sasa hawajakamatwa.

Hivi majuzi, Wizara ya Leba ilianza kupeana pesa za mpango wa Inua Jamii, baada ya kusubiri kwa miezi kadhaa. Chini ya mpango huo, mayatima, wazee, na wanaoishi na ulemavu hupewa KSh 2000 (38,000tsh) kila mwezi.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

Post a Comment

Previous Post Next Post