MAKAHABA WAPELEKANA MAHAKAMANI WAKIGOMBANIA MTEJA 'MMOJA ALISHUSHA BEI, KACHAPWA MANGUMI BALAA"

Mnamo Ijumaa, Disemba 9,2022 kahaba alifikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kumpiga kitutu mwenzake, mbele ya Hakimu Mkuu wa Mombasa.

Mariam Issa Mohammed aliyefika mbele ya Hakimu Mkuu Vincent Adet alikiri shtaka la kumpiga na kumjeruhi mwenzake Anita Mtengo.

Mahakama iliacha kinywa wazi baada ya Mariam kusimulia peupe chanzo cha ugomvi hadi kupigana kwa mangumi na mateke. 

Alisema kuwa yeye ni kahaba na mwathiriwa ni mwenzake wanaofanya kazi hiyo katika Soko la Sega, eneo la Majengo Mombasa.

Kulingana na Mariam, walitofautiana na mwenzake baada ya kushusha bei ya huduma kutoka bei ya kawaida ya KSh 350 (sawa na takribani shilingi shilingi 6000 ya Tanzania) hadi KSh 150 sawa na shilingi 3000 ya Tanzania)  na hivyo basi kumharibia biashara.

 Tukio hilo lilifanyika mnamo Jumatano, Disemba 7, kwa mujibu wa maelezo ya kesi hiyo. Wawili hao walikatizwa mara kwa mara na hakimu wakati walipoanza kubishana na kurushina maneno machafu ambayo hawapaswi kutamka ndani ya kortini.

"Mheshimiwa ni kweli mimi ni kahaba. Biashara hii inanilipia kodi ya nyumba na karo ya shule ya watoto wangu. Uzuri wa biashara hii ni kwamba unapata pesa za haraka mkononi," Mariam alisema kwa ujasiri. 

Mtengo aliiomba mahakama kumshurutisha mshatkiwa alipe gharama zote za matibabu, baada ya kumpiga kitutu na kumjeruhi. "Nimeumia sana na mkono wangu umejeruhiwa. Ninataka nilipwe fidia ya KSh 40,000 niliyotumia kwa matibabu," Mtengo alisema.

Chanzo - Tuko News

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments