ARGENTINA MABINGWA KOMBE LA DUNIA 2022...MESSI MCHEZAJI BORA



Mchezaji wa klabu ya PSG na timu ya Taifa ya Argentina Lionel Messi
****
TIMU ya Taifa ya Argentina imeibuka mabingwa kombe la Dunia kwa mikwaju ya Penati dhidi ya timu ya Taifa ya Ufaransa mara baada ya kutoka sare ya 2-2 kwa dakika 90 na 3-3 dakika 30 za nyongeza (extra time).

Argentina ilianza kutangulia kwa mabao 2-0, mabao yaliyofungwa kipindi cha kwanza kupita kwa nyota wao Lionel Messi pamoja na Angle Di Maria na kuwapeleka mapumziko wakiwa mbele.

Kipindi cha pili Ufaransa ilifanya mabadiliko ya baadhi ya wachezaji wake, mabadiliko ambayo yalizaa matunda kwani walipata mabao mawili ya haraka kupitia kwa kijana wao nyota Kylian Mbappe na kumfanya amzidi mpinzani wake Lionel Messi kufikia mabao saba wakati mweznake akiwa na mabao sita tu kwenye michuano hiyo.

Wakati huo huo Mchezaji wa klabu ya PSG na timu ya Taifa ya Argentina Lionel Messi ameibuka kuwa mchezaji bora wa mashindano ya Kombe la Dunia 2022 baada ya kufanikiwa kuisaidia timu yake ya Taifa kutinga Fainali na kunyakua kombe la michuano hiyo ambayo imepigwa nchini Qatar.


Messi pia amefanikiwa kushika nafasi ya pili kwa wafungaji wa mabao kwenye michuano hiyo akiwa na mabao saba huku Klyian Mbape akiibuka kuwa mfungaji bora akiwa na mabao nane

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments