MKURUGENZI MAIPAC : WAANDISHI WA HABARI ANDIKENI HABARI ZA KUISAIDIA JAMII







Mussa Juma Mkurugenzi Maipac na Mjumbe wa Bodi Misa- tan akitoa nasaha Kwa wahitimu na wageni katika chuo cha uandishi wa habari Fanikiwa Arusha yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika chuoni apo kilichopo mbauda ndani ya halmashauri ya jiji la Arusha

Mjumbe wa Bodi Fanikiwa Journalism School Arusha Elson Makaye kushoto akimkabidhi cheti Cha shukrani mgeni rasmi katika mahafali ya 16 ya chuo hicho yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika chuo hicho kilichopo Ndani ya halmashauri ya jiji la Arusha mkoani Arusha

Na Woinde Shizza ,Arusha
Waandishi wa habari nchini wametakiwa kuandika habari zenye manufaa Kwa jamii Kwa kuandika habari bunifu zinazolenga kuwakwamua wananchi kuondokana janga la umaskini.


Sekta ya habari na utangazaji ikitumika ipasavyo hususani vyombo vya habari mtandaoni kwa kuzingatia ukuaji wa teknolojia vinaharakisha zoezi la kuipasha jamii habari kwa wepesi na haraka zaidi hivyo kuwa chachu ya mabadiliko.


Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya wanahabari inayosaidia jamii za pembezoni nchini MAIPAC, Musa Juma alisema hayo wakati akihutubia wahitimu na wazazi katika mahafali ya 16 ya chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Fanikiwa Arusha yaliyofanyika hivi karibuni.


Alisema kuwa ulimwengu wa sasa umekua, haswa katika eneo la sayansi na teknolojia hivyo wana habari wanapaswa kukimbia na ukuaji huo wa teknolojia kwa kuandika habari bora na bunifu pia kuanzisha vyombo vya habari vya mitandaoni ambavyo vitawasaidia wao kujiajiri.


Hata hivyo ameeleza kuwa waandishi wengi wanaweza kufungua "Blog, radio mtandao na Tv za Mitandaoni ambazo wanaweza kupeleka maudhui mbali mbali ya kihabari na kupitia vyombo hvyo watapatikana wawekezaji mbalimbali ambao wataweka matangazo ya biashara zao ili zionekane na watazamaji au pengine wasomaji.


Musa Juma ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi MISA - TAN na Mkuu wa magazeti ya mwananchii Mkoani Arusha amewataka wahitimu hao wa ngazi ya Stashahada kuzingatia maadili wawapo kazini lakini pia kuwa wabunifu katika kuandika habari za mazingira, kilimo, uchumi, na mabadiliko ya TABIA NCHI ili kusaidia kuwaweka katika mazingira mazuri zaidi ya kihabari.


Naye mkuu wa chuo hicho Bwana Andrea Ngobole, amewataka wazazi wa wahitimu kuwaendeleza zaidi vijana hao katika chuo kikuu ili waendelee kupata elimu zaidi juu ya tasnia ya habari na sekta nyinginezo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments